BODABODA mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara
moja, mwanzoni mwa wiki hii alionja joto ya jiwe baada ya kuhenyeshwa na
polisi kufuatia kitendo chake cha kukataa kutii sheria bila shuruti,
alipotaka kusababisha ajali Barabara ya Chuo Kikuu, eneo la Mlimani
City, jijini Dar.
Dereva bodaboda akidhibitiwa na polisi.
Shuhuda wa sakata hilo aliliambia gazeti hili kuwa, mwendesha bodaboda
huyo aliyekuwa akitokea Mwenge kuelekea Chuo Kikuu, alisimama barabarani
ili kuzungumza na abiria aliyemsimamisha ndipo askari wa Jeshi la
Polisi wanaotembea na pikipiki, walimfuata na kuzungumza naye.
Dereva bodaboda akipambana na polisi.
“Polisi walimuuliza kwa nini amesimama barabarani kwani kitendo hicho
kingeweza kusababisha ajali, walimtaka awape funguo kwa kile
walichosema kitendo hicho ni ukiukwaji wa sheria, lakini bodaboda
alikuja juu na kuanza kutaka kupambana na polisi,” alisema shuhuda huyo.
Inadaiwa kuwa baada ya polisi hao waliokuwa na silaha zao za moto,
kuzozana kwa muda bila mafanikio na bodaboda huyo, walinzi wanaolinda
lango la kuingilia Mlimani City waliungana na polisi kumtaka mwendesha
pikipiki huyo kukubali kufuata sheria.
Wakimtia nguvuni.
“Baada ya kuona askari wa pikipiki na walinzi wamemzunguka mwenzao,
bodaboda mwingine naye alisogea na pikipiki yake pale ili aweze
kumsaidia, lakini naye akajikuta akiibwaga pasipo kufanikiwa kumnasua
dereva huyo ambaye alikuwa jeuri,” alisema shuhuda mwingine.Askari hao
walifanikiwa kumtaiti mwendesha bodaboda huyo na kwenda naye kituoni kwa
maelezo zaidi.
MSANII wa Bongo Fleva, Ali Kiba usiku wa kuamkia leo akiwa nyumbani
kwake Kunduchi jijini Dar es Salaam, alivamiwa na kundi la watu wapatao
20 wanaodhaniwa kuwa ni majambazi.
Ali Kiba akiwa katika pozi.
Watu hao waliokuwa na silaha za aina tofauti yakiwemo mapanga, visu
na silaha za moto walifanikiwa kuvunja kuingia ndani na kuwadhuru baadhi
ya ndugu wa Ali Kiba na kuiba mali na kila kitu ambacho waliweza
kubeba, walimpiga na kumtesa mlinzi wa nyumba hiyo wakimtaka awaonyeshe
alipo Ali Kiba, hata hivyo hawakufanikiwa kumpata na wakaondoka muda
mfupi kabla ya polisi hawajafika nyumbani kwa staa huyo baada ya
kupigiwa simu na majirani.
Ikiwa utakuwa na taarifa zozote zitakazosaidia kupatikana kwa
majambazi hao, unaweza kutoa taarifa katika kituo cha polisi ulicho
karibu nacho.
Ndugu wa marehemu waliouawa baadaya kukutwa na hatia yakuingiza madawa ya kulevya nchini Indonesia wakiwa ndani ya gari la wagonjwa liliobeba mwili ya ndugu yao mara baada ya kuupokea toka gerezani katika kisiwa cha Nusa Kambangan.
Indonesia imetetea uamuzi wake wenye
utata wa kuamua kuwauwa walanguzi wanane wa dawa za kulevya wakiwemo
raia saba wa kigeni, ikisema kuwa hivyo ni vita dhidi ya biashara ya
mihadarati.
Kwa upande wake, Australia imemuita nyumbani balozi
wake Nchini Indonesia, kama hatua ya kulalamikia kuuwawa kwa raia wake
wawili waliohusika na ulanguzi huo.
Waziri mkuu Tony Abbott,
anasema kuwa hata ingawa anaheshimu utawala wa Indonesia kama taifa
huru, uhusiano wa mataifa hayo mawili hautaendelea kama kawaida kufuatia
mauwaji ya wa-australia hao wawili.
Mkuu wa sheria Nchini Indonesia, Muhammad Prasetyo, ameelezea hatua hiyo ya Ausralia kama hasira za muda mfupi tu.
Moja ya majeneza ya wale waliouawa
Waustralia hao wawili waliuwawa kwa kupigwa risasi na kikosi maalum
cha wauwaji kwa pamoja na washukiwa wengine sita wa ulanguzi wa
mihadarati, watano kati yao walikuwa raia wa kigeni.
Licha ya vilio vya kuwasamehe watu hao kutoka kwa mataifa ya dunia, Indonesia iliamua kwa vyovyote kuwauwa.
Kuuwawa
kwa mfungwa wa tisa, raia wa Ufilipino, Mary Jane Veloso,
kumecheleweshwa na Rais Joko Widodo, baada ya mwanamke mmoja
kujiwasilisha kwa polisi nchini Ufilipino, akisema kuwa ndiye
aliyemhadaa mfungwa huyo mwanamke mwenzake, kupeleka dawa za kulevya
hadi Indonesia.
Brazil nayo inasema kuwa kuuwawa kwa raia wa pili
wa Brazil Nchini Indonesia, katika kipindi cha miezi minne, ni hatua ya
kutamausha na ambayo tayari imeyumbisha vibaya uhusiano wa kidiplomasia
wa mataifa hayo mawili.
Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR Mageuzi), David Kafulila akikabidhiwa Tuzo
ya utetezi wa haki za binadamu ya mwaka 2014, Mwenyekiti wa Tume ya
Haki za Binadamu na Utawala Bora Tom Nyanduga, Dar es Salaam jana.
Kulia ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini,
Martina Kabisama.
Dar es Salaam. Sakata la uchotwaji wa fedha
katika Akaunti ya Tegeta Escrow limemng’arisha Mbunge wa Kigoma Kusini
(NCCR- Mageuzi), David Kafulila baada ya kutunukiwa tuzo ya kutambua
mchango wake katika kufichua ufisadi huo uliohusisha uchotwaji wa Sh306
bilioni kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Katika sakata hilo, mawaziri wawili walipoteza
nyadhifa zao pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali baada ya Ripoti ya
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali kuwahusisha na sakata hilo.
Maofisa wengine kadhaa wa Serikali wamesimashwa au kufunguliwa mashtaka
kutokana na kuhusika kwao kwenye ufisadi huo.
Sakata hilo lililoteka kwa kiasi kikubwa mkutano
wa Bunge wa 16 na 17 kabla ya kufika bungeni, liliibuliwa na Gazeti la
The Citizen, linalochapishwa na Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd
na Kafulila kuwasilisha hoja ndani ya Bunge ili kujadiliwa.
Tuzo aliyopewa Kafulila jana na Mtandao wa
Watetezi wa Haki za Binadamu unaounganisha asasi za kiraia zinazotetea
haki za binadamu (THIRD-Coalition), ni moja kati ya tuzo tatu
zilizotolewa kwa Watanzania walioonyesha ujasiri katika kutetea haki za
binadamu nchini.
Wengine ni Maanda Ngoifiko wa asasi ya kiraia,
inayotetea haki za binadamu ya PWC kutoka Loliondo wilayani
Ngorongoro, na Mwandishi wa Gazeti la Mwananchi, Salma Said aliyetishiwa
kuuawa baada ya kuonyesha msimamo wa kukataa shinikizo la kukubaliana
na muundo wa Muungano wa serikali mbili wakati wa Bunge Maalumu la
Katiba.
Kwa mujibu wa THIRD-Coalition, vigezo
vilivyotumika kuwapata washindi hao vilizingatia mazingira ya kazi na
hali hatarishi aliyokutana nayo mshindi wa tuzo hiyo, ikiwamo taarifa
zilizokusanywa kupitia ripoti za matukio ya ukiukwaji wa haki za
binadamu kwa mwaka jana.
Baada ya kukabidhiwa, Kafulila alisema tuzo hiyo ni mwanzo wa hatua nyingine ya kuendelea kuibua ufisadi ndani ya Serikali.
“Nimepata ujasiri na kuamini kwamba siko peke
yangu katika vita hii, nashukuru kupata tuzo hii, lakini nashukuru zaidi
ushirikiano nilioupata kwa mhariri wa gazeti la The Citizen, ambaye
alinipatia nyaraka nne za kuanzia,” alisema Kafulila.
“Hata hivyo, ninasikitishwa kuona bado Tanesco
wakiendelea kulipia Dola 4 bilioni za capacity charge kwa kampuni hiyo
ya ITPL, wakati hukumu iliyotolewa na Mahakama ya ICSID ya Uingereza
Februari 12, mwaka jana inasema haikuwa sahihi tozo hiyo, lakini bado
kiwango hicho kinaendelea kulipiwa.”
Salma alisema pamoja na vitisho ambavyo bado
ameendelea kukutana navyo mpaka sasa kutoka kwa baadhi ya wabunge wa
lililokuwa Bunge la Katiba, bado msimamo wake utaendelea kuwa palepale.
Aidha, alisema vita iliyopo kwa sasa imehamia
kwenye harakati za Baraza la Katiba la Zanzibar ambalo linaendesha elimu
kwa Wazanzibari kuhusu Katiba Inayopendekezwa. “Mimi ni mjumbe wa
Baraza hilo na kwa sasa hawapendi kuona tukielimisha ukweli wa Katiba
hiyo na badala yake wanataka kueleza mazuri tu. Hilo tumesema
haliwezekani.”
Miswada ya sheria
Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na
Utawala Bora (THBUB), Tom Nyanduga aliyekabidhi tuzo hizo, amewataka
wadau wote wa haki za binadamu nchini kufungua kesi mahakamani kupinga
miswada hiyo itakayosainiwa na Rais wakati wowote kuanzia sasa.
Nyanduga aliwataka kutoendelea kulalamika tu na
badala yake wachukue hatua hiyo ili kujihakikishia haki imetenda kwani
Mahakama ndiyo sehemu itakayopima uhalali wa sheria hizo kama
zinawapokonya uhuru na haki zao kikatiba. Miswada hiyo ni ule wa Sheria
ya Takwimu ya mwaka 2015 na Sheria ya Makosa ya Mitandao ya mwaka 2015.
Kauli hiyo inajibu madai ya Jukwaa la Wahariri
Tanzania (TEF), kupitia viongozi wake, ambao juzi walisema ikiwa Rais
Jakaya Kikwete atasaini miswada hiyo kuwa sheria, watakwenda mahakamani
kupinga hatua hiyo licha ya Ikulu kueleza msimamo ikisisitiza kusainiwa
miswada hiyo.
Akizungumza jana wakati wa kusherehekea Siku ya
Watetezi wa Haki za Binadamu nchini, jijini hapa, Nyanduga alisema:
“Wasilalamike tu kuna utaratibu ambao wanaweza kufikisha madai yao
mahakamani bila kujali kama rais atasaini au la kwani yeye (Rais) anayo
mamlaka yake kikatiba,ila wakienda mahakamani haki itatendeka kama kuna
ukandamizaji umefanyika,” alisema Nyanduga.
Mbali na utoaji wa tuzo hizo, umoja huo pia
ulizindua ripoti ya taarifa ya hali ya upiganiaji wa haki za binadamu
kwa mwaka 2014, ambayo inaonyesha kuwa kesi tano zilifikishwa
mahakamani, kesi 20 zilizoripotiwa na waandishi mbalimbali wa habari
nchni, wakidai kufanyiwa vitisho huku ikielezea maombi ya uboreshaji wa
sheria 29 kandamizi katika uhuru na haki za wananchi kupata taarifa.
Mwenyekiti wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu
(LHRC), Dk Hellen Kijo Bisimba alikuwa miongoni mwa wadau wa umoja huo
ambaye alisema kundi la wanaokandamiza haki isitendeke nchini linazidi
kujitokeza, huku likijenga hofu kwa watetezi wa haki.
“Kundi hilo halipendi kukosolewa na hata likiona
kuna utetezi sehemu fulani, basi yule anayetetea atakuwa kwenye wakati
mgumu. Mfano kuna vipingamizi vya kuzuiwa na wakuu wa wilaya, wakuu wa
mikoa ili tusitoe elimu juu ya Katiba inayopendekezwa katika baadhi ya
wilaya nchini. Hatuwezi kukubaliana na hali hiyo lazima tuone haki
ikitendeka kwa wote,” alisema Dk Hellen.
Jeshi la Nigeria limesema limewaokoa
watoto wa kike mia mbili na tisini na tatu kutoka katika kambi ya Boko
Haram iliyoko katika msitu wa Sambisa, kaskazini mashariki mwa nchi
hiyo. Jeshi hilo limesema watoto hao waliokolewa si kati ya wale
waliotekwa mwaka mmoja uliopita na kundi la kiislamu katika eneo la
Chibok.
Jeshi limeiambia BBC kwamba wanawake na watoto hao wa kike
walikutwa katika kambi nne tofauti ambapo silaha pia
zimekamatwa,Msemaji wa jeshi amesema waliwapata wasichana hao baada ya
kuziharibu kambi hizo.
"ni muda mfupi tu uliopita, wanajeshi wetu
wameingia katika msitu wa Sambisa, kutokea upande wa Alafa, ambapo
walikuta kambi nne zinazomilikiwa na wapiganaji na kuziharibu, hapo
ndipo walipogundua kuwa kuna wasichana wapatao mia mbili na wanawake
tisini na tatu." Kwa
sasa jeshi limezuiwa kutoa utambulisho wa wasichana hao. Hata hivyo,
jeshi limethibitisha kwamba wasichana hao sio wale wanafunzi waliotekwa
katika mji wa Chibok.
"tuko katika mchakato wa kuwachunguza hawa
wasichana ili tuweze kubaini utambulisho wao, lakini kitu kimoja nataka
nikiweke wazi kwa umma, tunapotaja idadi ya wasichana mia mbili, tayari
watu wanaanza kufikiria wasichana mia mbili wa Chibok waliotekwa mwaka
jana, hawa sio wasichana wa Chibok, tutaendelea kuwajuza kadri muda
unavyokwenda iwapo kutakuwa na taarifa zozote. "
Waziri wa
Nishati na Madini, George Simbachawene (kulia) akipata maelezo kwa
wakurugenzi wa kampuni ya Tanzanite One, Faisal Juma Shabhai na Hussein
Gonga
Arusha, Kampuni ya Tanzanite One ambayo sasa inamilikiwa na
wazawa, imeongeza ajira kwa vijana kutoka 700 hadi 1,280 ili kukabiliana
na tatizo hilo nchini.
Wakizungumza na waandishi wa habari katika
maonyesho ya madini ya vito yanayoendelea jijini hapa, wakurugenzi wa
Kampuni ya Sky Associate Ltd iliyonunua asilimia 50 ya hisa ndani ya
Tanzanite one, Hussein Gonga na Faisal Juma walisema wameanzisha pia
mafunzo ya kukata kna usanifu wa madini.
Gonga alisema Sky Associate na Shirika
linaloshughulikia Madini Tanzania (Stamico) ambao ndiyo wamiliki wa
Tanzanite One, wameongeza maeneo ya uchimbaji madini ili kuhakikisha
wanaongeza ajira kwa vijana wengi wanaotafuta ajira za uchimbaji katika
migodi ya madini.
Alisema katika mafunzo ya ukataji na usanifu wa
madini, vijana hufundishwa jinsi ya kuyaongezea thamani na wanaohitimu
hupatiwa mashine.
Awali, Mkurugenzi mwenza wa Tanzanite One, Faisal
Juma alisema mipango ya kuongeza ajira na kutoa mafunzo ya usanifu wa
madini itasaidia kuboresha sekta ya madini nchini.
Juma alisema Tanzanite One kama kampuni kubwa
nchini ya uchimbaji wa madini ya vito, itahakikisha inashirikiana na
Serikali na wadau wengine kufanya mapinduzi katika sekta ya madini ili
Watanzania wengi waweze kunufaika.
Kamishna wa Madini Tanzania, Paul Masanja
akizungumza katika maonyesho hayo, aliwataka wamiliki wa migodi na
wachimbaji kushirikiana kuboresha sekta ya madini kwa kuhakikisha
hawauzi wa kuyatorosha nje ya nchi madini ghafi.
Alisema Serikali itaendelea kushirikiana na wadau
wa madini kuhakikisha wanapata masoko ya madini yao na alipongeza
jitihada za kuwapa mafunzo vijana juu ya ukataji wa madini.
• Tycoons Tanil Somaiya & Rostam Aziz implicated in the scam • Vodacom Tanzania MD Rene Meza receives $5 million bribe to keep silent • Tax worth over 121.5 billion/- evaded in the deal • PCCB, TCRA, TRA caught napping in massive fraud bigger than EPA and Escrow combined
A staggering $350 million (over 675 billion shillings) was stolen
from Tanzanians in a massive scandal involving the sale of pirated
electronic recharge vouchers from Vodacom Tanzania to customers.
The scam, which is bigger than the Bank of Tanzania’s infamous
external payment arrears (EPA) and IPTL Tegeta escrow account scandals
combined, involves Tanil Somaiya, a business tycoon behind several
dubious deals in Tanzania, including the military radar transaction with
Britain’s BAE Systems.
The production of the electronic recharge vouchers followed the
signing of a contract between Vodacom Tanzania and Tanil’s Shivacom
Group in 2007/08. This means that Shivacom acted both as a Vodacom super
dealer and printer and supplier of electronic recharge vouchers, an
obvious conflict of interest.
In the elaborate scandal, Tanil’s company, Shivacom Group, printed
millions of pirated 500 shillings electronic recharge vouchers (Jero
Jero) between 2008 and 2012 and colluded with other companies owned by
Fred Lowassa (Alphatel) and TIB Development Bank Managing Director Peter
Noni (Planetel) to distribute the vouchers across Tanzania.
Fred Lowassa is the director of Alphatel, a Vodacom super dealer,
while Noni, a former senior Bank of Tanzania (BoT) official, also owns
another Vodacom super dealer, Planetel.
Together, Shivacom colluded with Alphatel and Planetel to carry out
the massive fraud involving the production, distribution and sale of
pirate electronic recharge vouchers worth over 675 billion shillings
without Vodacom’s knowledge until the scam was unearthed in 2012.
There was also rampant tax evasion in the scandal with Value Added
Tax (VAT) worth more than 121 billion shillings evaded by Shivacom and
its conspirators, which is a serious criminal offence.
Senior officials at Tanzania government regulatory and watchdog
agencies such as the Tanzania Revenue Authority (TRA), the Tanzania
Communications Regulatory Authority (TCRA) and the Prevention and
Combating of Corruption Bureau (PCCB) were either complicit in the
scandal or were caught napping.
Shivacom alone distributed more than half of the fake recharge
vouchers, while the other pirate vouchers were distributed by its
conspirators — Alphatel and Planetel.
The “Jero Jero” vouchers are the most fast-moving electronic recharge
vouchers in Tanzania, with Shivacom printing hundreds of millions of
fake vouchers using pins provided by Vodacom Tanzania.
The scandal not only caused Vodacom Tanzania huge financial loss, it
also resulted in the detrimental loss of customer confidence. This is
partly attributed to Vodacom Tanzania losing its dominance in Tanzania’s
mobile phone industry, with Airtel and Tigo now threatening to wrestle
away the company’s market share.
Insiders say Vodacom Tanzania’s MD, Rene Meza, found out about the
scandal after just arriving in Tanzania from Kenya to take up the
position of Vodacom Tanzania managing director.
“Rene Meza confronted Tanil about the scandal and demanded a $10
million kickback to keep quiet. Tanil arrogantly told him to piss off,
so Rene retaliated by instructing Vodacom’s legal counsel to write a
letter to Shivacom to terminate the electronic recharge voucher
agreement for breach of contract,” said a well-placed source.
“Tanil went to Vodacom South Africa’s Group CEO, Shameel, and gave
him a bribe of $400,000. Shameel then instructed Vodacom Tanzania to
settle the matter with Shivacom. Rene Meza finally settled for a $5
million bribe from Tanil and Vodacom paid Tanil hefty compensation for
termination of the contract despite the obvious fraud.”
Vodacom Tanzania’s lawyers gave legal advice that the contract should
be terminated and Shivacom should pay compensation to Vodacom for the
fraud. However, after bribes exchanged hands, Shivacom ended being paid a
hefty compensation by Vodacom despite perpetrating the massive fraud.
In all this scandal, Tanil used a Dar es Salaam-based lawyer, Dilip Kesaria, to respond to legal queries from Vodacom.
Kesaria, who was disbarred in the United Kingdom for malpractices but
fraudulently allowed to operate as a lawyer in Tanzania, is the
Principal at Kesaria & Company advocates.
The following is a chronology of key events in the massive 675
billion shillings fraud involving Vodacom Tanzania’s Jero Jero
electronic recharge vouchers: Key Facts and Figures • 2008. A 10-year agreement comes into effect for
Shivacom Tanzania Limited to provide electronic recharge vouchers (EVD)
to Vodacom Tanzania Limited. This means that Shivacom effectively played
a dual role of being a Vodacom super dealer and EVD supplier in
separate agreements. • 2008-2012. The massive fraud committed by Shivacom
over the 5-year period is worth more than $350 million (675 billion
Tanzanian shillings), which is bigger than the Bank of Tanzania EPA and
Tegeta Escrow account scandals combined. This fraud was done by Shivacom
printing TZS 500 electronic recharge vouchers (Jero Jero) fraudulently
and distributing them into the market without Vodacom’s knowledge.
Other Vodacom super dealers, including Alphatel and Planetel are also
implicated in directly colluding with Shivacom to distribute pirate
recharge vouchers. • 31 July 2012. Vodacom Tanzania Ltd’s Chief Legal
& Regulatory Officer writes a letter to Shivacom Tanzania Ltd to
formally notify the company about breach of contract. This comes after
Vodacom Tanzania Ltd discovered that Shivacom has been engaged in
massive fraud over the past 5 years (2008-2012) by printing and
distributing pirate electronic recharge vouchers using pin numbers
provided by Vodacom. This letter effectively terminated the EVD contract
between Vodacom Tanzania Ltd and Shivacom Ltd. • 3 August 2012. Shivacom responds to Vodacom’s letter, disputing the decision to terminate the EVD contract under advice from Kesaria. • 3 September 2012. Shivacom Group’s Managing
Director, Tanil Somaiya, writes a letter to Vodacom’s Group CEO in South
Africa, Shameel Aziz Joosub, requesting a meeting to discuss the EVD
contract termination. Tanil succeeds in meeting with Shameeel, who is
compromised and orders Vodacom Tanzania to settle the matter with
Shivacom and pay compensation to the company for contract termination
despite the fraud. The meeting between Tanil and Shameel with other
senior Vodacom officials took place on 1 November 2012.
Vodacom Tanzania MD, Rene Meza, receives a bribe of $5 million from Tanil Somaiya to resolve the matter. • 9 November 2012. Tanil writes a letter to Shameel,
saying he was offering his Shivacom Superdealership subscriber base for
sale. Shivacom gave Vodacom the right of first refusal and asked for
consent to scout around for alternative buyers if Vodacom was not
interested in buying the dealership. • 14 November 2012. Vodacom Tanzania Ltd’s Chief
Legal & Regulatory Officer writes a letter to Shivacom offering
compensation payment for termination of the contract. This is despite
the fact that Vodacom’s lawyers gave legal advice to the firm to
terminate the contract with Shivacom given the fact that Shivacom have
breached the contract by duplicating TZS 500 vouchers. • 29 November 2012. Tanil writes a letter to Shameel
rejecting Vodacom’s “paltry” compensation offer. Tanil demands hefty
compensation for loss of profit, cost of hardware and software of the
voucher production equipment and cost of unutilized stock of raw
materials. • 2012-2015. Vodacom settles with Shivacom by paying
the company a multi-million U.S. dollar compensation despite the
company committing the massive fraud. To be continued…
Helikopta iliyotumiwa na Kada wa CCM Buni Ramolle, ikitua katika Uwanja wa Pasua mjini Moshi, Aprili 18 mwaka huu.
Moshi. Helkopta ya Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo,
imeleta kizaazaa, baada ya Kada wa CCM, Buni Ramolle ambaye aliikodi kwa
ajili ya mikutano yake ya kutangaza nia ya kugombea ubunge katika jimbo
hilo, kudai kuwa ni mbovu na ilitaka kumuua.
Kada huyo akaenda mbali na kueleza kuwa kutokana
na hitilafu hiyo, ameitaka kampuni ya General Aviation Services (T) Ltd,
iliyomkodishia helkopta hiyo, kumrejeshea fedha zake zote alizoilipa
kwa ajili ya kuitumia wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu unaotarajiwa
kufanyika Oktoba mwaka huu.
Hata hivyo, Ndesamburo ambaye ni mmiliki wa
helkopta hiyo kupitia kampuni yake ya Keys Aviation, alikanusha madai
hayo akisema kuwa hayana msingi.
“Anasema helikopta ni mbovu wakati ilimpeleka na
kumrudisha? Alihoji Ndesamburo na kusisitiza kuwa “tutawaomba wakaguzi
wa ndege waifanyie ukaguzi na ripoti hiyo ndio tutaitumia kumshitaki
nayo.”
Kuhusu madai ya Ramolle kuwa amerejeshewa fedha
zake alizolipa, Ndesamburo alihoji “Tunamrudishia fedha gani wakati
hakulipa? Kuwa na Proforma Invoice ndio kulipia?”
Awali taarifa zilieleza kuwa Ramolle alitoa tuhuma
hizo, baada ya viongozi wa CCM, kumbana wakimtaka aeleze kwa nini
ameamua kutumia helkopta ya Ndesamburo ambaye ni mpinzani wake kisiasa.
Jana Ramolle alitumia mkutano wake na waandishi wa
habari kukanusha kuwa helkopta aliyoitumia Aprili 18 mwaka huu ni ya
Ndesamburo. Alidai katika mkutano huo kuwa helkopta hiyo aliikodisha
kama mteja kutoka kampuni ya General Aviation Services na hajui kama ni
ya Ndesamburo.
Lakini tayari Ndesamburo mwenyewe ameshajitokeza
hadharani na kudai kuwa helkopta hiyo ni mali yake na kwamba ameingia
mkataba wa kuikodisha kwa kampuni ya General Aviation Services (T) Ltd.
Huu ni mchezo mchafu
Kwa mujibu wa Ramolle, kinachofanyika sasa ni
mbinu za kumchafua ndani ya chama ili asiaminike na aenguliwe kama
alivyoenguliwa mwaka 2010.
Ramolle alisema kutokana na Ndesamburo kudai
helkopta hiyo ni yake, tayari kampuni ya General Aviation Services
wamemrudishia fedha zake alizokuwa amekodishia na ameishtaki kampuni
hiyo kwa Meneja wa TRA mkoa wa Kilimanjaro kutokana na kutompa risiti ya
malipo aliyoyafanya. Buni alisema atapambana na waandishi wanaotaka
kumchafua kwa kuwa ana mahasimu ndani na nje ya chama na kutaka
asiharibiwe kazi yake na siasa.
“Nimechoka kunyanyaswa nimepata madhara makubwa
kwa sababu ya siasa nina maadui ndani na nje ya chama nitapambana na
yeyote atakayenizushia maneno na mtu asinifuatefuate” alisema.
Akizungumzia kutumia chopa kwenye mikutano,
Ramolle alisema nia ni kuleta ushawishi kwa wananchi ili wahudhurie
mikutano na kwamba hekopta si maendeleo.
“Nimechukua (chopa) makusudi ili kuwaonyesha
wananchi Chopa si maendeleo, watu wa Moshi wanafikiri chopa ni maendeleo
chopa kazi yake ni kuvuta watu na nimeshaiagiza itakuja hii
niliyokodisha awali ni mbovu kwanza ingeweza kuniua ile,” alisema.
“Nilitaka watu wajue chopa siyo maendeleo, Ndesamburo alikuwa akiitumia kuwavuta tu. Maendeleo ni uwajibikaji”
Ramolle alisema kwa maslahi ya watu wa Moshi yupo
tayari kuchukua uamuzi mgumu iwapo chama kitaengua jina lake .
“Nikishinda halafu jina langu likakatwa patachimbika.”
Bruce Jenner aliyekuwa mwariadha
bora duaniani kabla ya kuwa nyota wa kipindi cha televisheni na familia
moja maarufu duniani ''The Kardashians''. sasa amefichua siri ambayo
amekuwa akiificha kwa miaka mingi.
''Kwa nia na madhumuni yote,
mimi ni mwanamke.'' Jenner aliambia Sawyer kutoka ABC katika mahojiano
maalum yaliopeperushwa hewani siku ya Ijumaa.
''Watu wananiona
tofauti,wananiona kama mwanaume, lakini moyo na roho yangu na kila kitu
ninachofanya maishani ni sehemu yangu.'' Jenner ambaye ana umri wa miaka
65 amesema. '' Upande huu wa kike ni sehemu yangu.
hivi ndivyo mimi nilivyo.''
Katika masaa ya mahojiano na Diane Sawyer mjini New York na
California, Jenner alielezea kwa kina mapambano yake ya kuwa na jinsia
mbili tangu utotoni.
''Akili zangu ni za kike sana kuliko za
kiume.'' Ameongezea. '' Ni vigumu sana watu kuelewa, lakini hivyo ndivyo
nafsi yangu ilivyo.''
Jenner aliyejawa na hisia na mwenye nywele
ndefu shati na suruali ndefu alisema kuwa amesubiri kwa miaka mingi ili
kujitangaza kwa kuwa hakutaka kuwavunja moyo watu.
Kwa miongo
kadhaa wake wa zamani wa Jenner na madada zake waliweka siri kuhusu
jinsia yake na kwamba walikuwa watu waliokuwa wakijua siri hiyo.
Mtandao wa watu wanaojua siri hiyo hatahivyo ulipanuka hivi majuzi wakati Jenner alipomwambia mamaake na wanawe 10 .
Jenner
ana watoto sita Burt,Cassandra,Brabdon,Brody,Kendall na Kylie pamoja na
watoto wanne wa kambo akiwemo Kourtney,Kim,Khloe na Rob Kardashian.
Yanga imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa kuifunga
Polisi Morogoro mabao 4-1 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, licha ya
kuwa imesaliwa na mechi kadhaa kumaliza msimu wa 2014/2015. Wafungaji wa
mabao ya Yanga leo ni Amiss Tambwe aliyefunga hat trick na Simon Msuva.
Imekuwa ikielezwa kuwa wasanii ni kioo cha jamii. Kwa maana hiyo
wanatakiwa kufanya mambo ambayo yanaweza kuigwa na wale wanaowatazama.
Hata hivyo, maisha wanayoishi baadhi ya wasanii hayaakisi msemo huo.
Wengi wamekuwa wakikumbwa na skendo mbalimbali zinazowafanya wasiwe na vigezo vya kuitwa kioo cha jamii.
Miongoni mwa mambo yanayowafanya wakati mwingine wadharaulike ni
kutoa maneno machafu, ‘live’ au kupitia kwenye mitandao ya kijamii.
Katika makala haya nitawazungumzia mastaa wanaoongoza kwa kutukana
mitandaoni lakini pia wale ambao wanaongoza kwa kutukanwa katika siku za
hivi karibuni.
Wastara Juma
Wastara…
Huyu
Wastara amekuwa akiheshimika kwenye jamii kwa muda mrefu na alikuwa ni
miongoni mwa mastaa wa kike ambao wangesimama na kuamua jambo
wangesikilizwa kutokana na jinsi alivyokuwa amejiweka na kuwaaminisha
watu.
Lakini katika siku za hivi karibuni alichafuka kwa kuingia katika
orodha ya mastaa wanaotukana mtandaoni baada ya kumvaa mmoja wa
mashabiki wake aliyemsemea mbovu na kumtukana matusi mazito
“Iweje anakubali kushushwa na mtu mmoja ambaye alikaa na kuamua
kumvuruga, anasahau kama kuna kundi la watu linamheshimu?” Aliandika
mmoja wa mashabiki wake kwenye mtandao wa Instagram baada ya kuona
matusi hayo.
Amanda Posh
Wafuatiliaji wa mambo na hasa wale ambao wapo Facebook watakumbuka
jinsi staa huyu wa filamu alivyomshambulia jamaa mmoja aliyefahamika kwa
jina la Joel.
Haikuwa ustaarabu kabisa kwa staa huyo kufanya hivyo kwani jambo
lililomkasirisha angeweza kulipuuza na angebaki na heshima yake huku
yule aliyemtukana akionekana mjinga.
Lakini ukiacha hilo, Amanda amekuwa akisifika kwa kutoa maneno
machafu pale anapochokozwa, tabia inayomfanya afiti kwenye makala haya.
Isabela Mpanda
Katika mastaa micharuko, huyu yumo! Hajivuni, hajisikii lakini ukimchokoza lazima akushikishe adabu kwa matusi.
Posti zake zenye lugha chafu kwenye mtandao wa Instagram zipo nyingi
lakini pia kwa wale wenye kumbukumbu watakumbuka kuwa staa huyu aliwahi
kumtukana mwanamitindo Belina Mgeni na mpaka sasa hawaongei.
Hao ni baadhi ya mastaa ambao katika siku za hivi karibuni wameshika chati kwenye suala la kutukana mtandaoni.
Kwa upande wa wale ambao wanashika nafasi za juu kwa kutukanwa, wapo wengi lakini leo tutawazungumzia wahanga watatu.
Kajala Masanja:
Tangu
aingie kwenye bifu na Wema Sepetu, kuna kundi ambalo linajiita Team
Wema limekuwa likimshambulia kwa kumtukana na kumshutumu kwa mambo
ambayo mengine hayana ukweli.
Hata hivyo, Kajala anaonekana kuwa mstaarabu kidogo kwani licha ya
kutukanwa mtandaoni, yeye amekuwa mkimya akijua kujibizana na watu hao
ambao wala hawana majina ni sawa na kuzidi kujichafulia. Elizabeth Michael ‘Lulu’: Huyu naye ni mhanga wa matusi
mtandaoni. Kuna kundi la watu ambao linaonekana kuwa na chuki dhidi
yake, huenda kutokana na mafanikio aliyonayo akiwa kwenye umri mdogo.
Lakini
sasa, licha ya matusi anayoyaoga mtandaoni, amekuwa mvumilivu wa
kuyaacha yapite. Watu wake wa karibu wanaeleza kuwa, licha ya kutukana
sana mwenyewe wala hajui kwamba anatukanwa kwani si mtu wa kufuatilia
nani kasema nini kibaya juu yake Wema Sepetu:
Kama ilivyo kwa Kajala, huyu naye anashambuliwa sana na Team Kajala.
Hawa ni watu ambao wamejitenga kuhakikisha wanamkosesha amani staa huyu.
Amekuwa akitukanwa kwa mengi lakini kwa kuwa anajua ustaa ni kama jalala, huwa hajali na anachukulia poa.
Ni mara chache sana amekuwa akinyanyua mdomo wake kuwajibu wale ambao wamekuwa wakimsema vibaya sambamba na kumtukana.
Kwa uchache hao ndiyo mastaa ambao hivi karibuni wametia fora kwa
kutukana na kutukanwa mtandaoni. Tahadhari Mastaa ambao ni wepesi kutukana mtandaoni wajue kwamba endapo
Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete atasaini ile
sheria ya makosa ya mtandaoni ya mwaka 2015, watajikuta wanaenda jela
hivi hivi.
"Tunashangazwa na jaji Mtungi kwa
kubadili jina la chama chetu bila ya kufuata taratibu huku akijua fika
kuna kesi ya msingi ipo mahakama kuhusu mwenendo wa chama hicho. Alisema
Limbu
Aliongeza kuwa kuna njama za makusudi zilizofanywa za
kubadilisha jina la chama hicho kwani haiwezeka na haiingii akilini
kubadilisha jina la chama kwa kipindi kifupi na haraka kiasi hicho.
"ACT-Tanzania ni chama chetu sio cha Zitto na kama anahitahi siasa safi
aanzishe chama chake kwani nafasi hiyo ipo wazi kwa kila mtanzania.
Alisema ni jambo la ajabu kuona chama kinafanya mkutano wake mkuu wenye
nia hofu na kumpatia mtu madaraka ya kioongozi mkuu na kubadilisha jina
lake huku msajili wa vyama akishuhudia.
Alisema msajili wa
vyama vya siasa alitoa tamko la kubadilishwa jina la chama hicho tarehe
20-4-2015 wakati tayari kiongozi mkuu wa chama hicho kilichobadilishwa
jina akiwa katika zaira ya kichama mikoani aliyoianza tarehe 10-4-2015
huku wakigawa kadi kwa kupitia chama cha ATC-Wazalendo.
Limbu
alihoji fedha zinazotumika kwenye ziara hiyo na za kuchapa kadi, bendera
za chama na vifaa vingine kuwa zinatoka wapi kama hakuna watu wenye nia
mbaya na chama cha ATC-Tanzania. (Imeandaliwa na mtandao wa http://www.habarizajamii.com/)
Diamond akilibusu tumbo la mpenzi wake Zari ambaye ni mjamzito.…
Mwanamuziki Nasibu Abdul 'Diamond' akijiachia na mpenzi wake Zarinah Hassan 'The Boss Lady' Visiwani Zanzibar.
Mwanamuziki Nasibu Abdul 'Diamond' akijiachia na mpenzi wake Zarinah Hassan 'The Boss Lady' Visiwani Zanzibar.
STAA
wa Bongo Fleva nchini, Nasibu Abdul 'Diamond' na mpenzi wake Zarinah
Hassan 'The Boss Lady' wamezidi kuonyesha kuwa penzi lao linazidi
kuimarika baada ya Zari kuachia picha Instagram wakiwa 'close'
walipokwenda Visiwani Zanzibar juzi.
Wapenzi hao walikuwa Zanzibar kwa ajili ya shoo ya Diamond iliyofanyika Jumamosi (Aprili 25, mwaka huu) usiku huko Ngome Kongwe.
Mojawapo ya picha za wapendanao hao imbayo imeenea mitandaoni ni ile
ambayo Diamond analibusu tumbo la Zari mwenye ujauzito unaodaiwa kuwa wa
staa huyo.
Makomandoo wakipita kwa ukakamavu mbele ya Rais Jakaya Kikwete wakati wa
kuadhimisha miaka 51 ya Muungano kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam
jana.
Dar es Salaam. Tanzania jana iliadhimisha miaka 51 ya Muungano
wa Tanganyika na Zanzibar huku viongozi wa upinzani wakisusia sherehe
hizo za mwisho katika utawala wa Rais Jakaya Kikwete ambazo, makomandoo
wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), walitia fora.
Rais Kikwete alikagua gwaride hilo katika sherehe zilizofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na kuhudhuriwa na
viongozi mbalimbali pamoja na maelfu ya wananchi
ambao baadhi walilazimika kutumia Uwanja Mkuu wa Taifa kufuatilia
shughuli hizo.
Baadhi ya viongozi hao ni pamoja na, Makamu wa
Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal, Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein,
Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim
Seif Sharrif Hamad. Wengine ni Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, Rais
mstaafu wa awamu ya sita wa Zanzibar, Amani Abeid Karume na Waziri Mkuu
Mstaafu, Frederick Sumaye.
Wapinzani wasusia
Viongozi wakuu wa vyama vya upinzani hawakushiriki
maadhimisho hayo baadhi wakiwa mikoani katika shughuli za kuimarisha
vyama vyao kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), Freeman Mbowe yuko mkoani Kagera na Mwenyekiti wa Chama cha
Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba ambaye yuko mkoani Mtwara.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James
Mbatia, Kiongozi wa ACT – Wazalendo, Zitto Kabwe hawakuhudhuria na
sababu za kutokuwapo kwao hazikuelezwa.
Wakuu waliokosekana
Pia, baadhi ya viongozi wa kitaifa hawakuonekana
katika sherehe hizo akiwamo Rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan
Mwinyi, Mawaziri wakuu wa zamani, Jaji Joseph Sinde Warioba, John
Malecela, Salim Ahmed Salim, Cleopa Msuya, Edward Lowassa.
Kikwete uwanjani
Kama ilivyo kawaida, msafara wa Rais Kikwete
aliyekuwa na Mkuu wa Majeshi, Davis Mwamunyange katika gari maalumu la
jeshi lililozungukwa na magari mengine saba na pikipiki 15, ulizunguka
uwanja huku kiongozi huyo akipunga mkono na kushangiliwa kwa nguvu.
Hatua hiyo ilifuatiwa na wimbo wa Taifa sambamba na mizinga 21
na kisha Rais Kikwete ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu alikagua gwaride la
vikosi vya ulinzi na usalama.
Hata hivyo, wakati akikagua gwaride hilo, Rais
Kikwete alipofika kwenye Kikosi cha Bendera, alisahau kupokea heshima
hali iliyomfanya arudi nyuma kufanya hivyo kisha kuendelea kukagua
vikosi vingine.
Baada ya hapo, ndege za kivita zilipita juu ya
uwanja zikitokea Kaskazini kulekea Kusini mwa uwanja. Tukio hilo
liliwafanya wananchi waliofurika katika uwanja huo kushangilia hasa kwa
jinsi ndege hizo kivita zilivyokuwa zikifanya madoido angani.
Ndege hizo zilifuatiwa na gwaride la nje
lililokuwa na vikosi 13 vikiongozwa na bendera ya Rais na ile ya JWTZ
zilizokuwa sambamba na bendera saba, sita zikiwa ni za vikosi vya
majeshi ya ulinzi na usalama pamoja na ya kikundi cha usindikizaji.
Vilipita mbele ya Rais kwa mwendo wa haraka. Baadaye Vilifuata vikosi
viwili; Kikosi Maalumu cha Wanamaji (Marine Special Force) na makomandoo
vikiwa katika mwendo wa mchakamchaka.
Baada ya makomandoo kupita, alifuata askari polisi
mmoja wa jeshi (MP) aliyepita peke yake kwa mwendo wa ‘digidigi’ na
kushangiliwa kwa nguvu.
Makomandoo
Sherehe hizo zilikuwa na mvuto wa aina yake kutokana na manjonjo ya makomandoo hao walipokuwa wakipita mbele ya Rais Kikwete.
Kikosi cha makomandoo hao kikiwa katika mavazi ya
kivita, bunduki, mabegi mgongoni hukuwa wakiwa wamepaka rangi nyuso zao,
waliingia huku wakikimbia mchakamchaka na kushangiliwa kwa nguvu.
Halaiki
Sambamba na makomandoo, halaiki ya watoto
iliyoonyesha mafunzo katika meli ya kivita nayo iliwanyanyua wananchi
katika viti vyao kushangilia huku waliokaa jukwaa kuu wakiinua bendera
na kuzipepea.
Halaiki hiyo iliyoingia uwanjani saa 5.10 ilianza
kwa kutoa ujumbe wa sherehe hizo kwa mwaka huu ambao ni “Miaka 51 ya
Muungano, Tudumishe Amani na Umoja, Ipigie Kura ya Ndiyo Katiba
Inayopendekezwa na Kushiriki Uchaguzi Mkuu.” Kisha kuhamasisha kilimo
wakisisitiza matumizi ya zana za kisasa. Pia, watoto hao wa halaiki
walitoa ujumbe kupinga ujangili katika mbuga za wanyama ili kulinda
maliasili hiyo kwa ajili ya vizazi vijavyo. Kadhalika, walihamasisha
ujasiriamali wa kutumia kazi za mikono.
Kivutio kikubwa katika halaiki hiyo ilikuwa ni
jinsi watoto hao walivyohamasisha ulinzi ambako walitoa ujumbe kuwa
suala hilo ni jukumu la wananchi wote. Wakati wanatoa ujumbe huo
walikuwa katika mwendo wa haraka huku wakienda mbele na nyuma na kutoa
burudani nzuri kwa hadhira iliyokuwepo uwanjani hapo pamoja na
watazamaji kupitia runinga.
Wakiendelea na onyesho la ulinzi, watoto hao walipita katika
vikwazo huku wakiruka na kupita katikati ya maduara makubwa ya vyuma
yaliyokuwa yanawaka moto na kisha kukanyaga makarai yaliyokuwa na moto
pia.
Pia kulikuwa na watoto watatu waliopita juu ya
kamba kwa staili tofauti na kuwavutia wazazi waliokuwapo. Wa kwanza
alipita huku akining’inia kwa mikono yake. Alifuatiwa na aliyeshika
kamba kwa mikono pamoja na miguu; uso ukielekezwa angani. Wa mwisho
alipita juu ya kamba hiyo kwa kutambaa.
Mazoezi mengine ni yake ya mfano wa meli ya kivita
yaliyokuwa yameandaliwa kwa umakini mkubwa. Watoto hao walipanda mnara
wa meli hiyo kwa aina tofauti. Kuna aliyepanda kwa mikono pasipo miguu
yake kugusa nguzo. Mwingine alipanda huku miguu yake ikiwa imenyooka
mbele na wa mwisho alipanda kwa kuruka ruka.
Wakiwa bado ndani ya meli hiyo, mmoja alijifunga
kamba mguuni na kuwanyanyua wenzake wawili kutoka chini. Ilikuwa ni
mithili ya filamu nzuri ya kivita.
Kabla hawajaondoka, walipita katika mfumo wa
vifaru vya kivita. Kimoja kikiwa cha kupiga masafa marefu na kingine
mafupi. Watoto watatu walitengeneza matairi ya vifaru hivyo. Usingependa
kuondoka wala kutaka watoto hao wamalize kuburudisha. Kwa hakika
walivutia.
Ngoma, Kwaya
Baada ya halaiki zilifuata ngoma za makabila.
Ngoma nne zilitumbuiza, mbili kutoka visiwani na nyingine bara. Pia
kwaya kutoka Chunya, Mbeya ambayo ilifuatiwa na wimbo maalumu.
Wapongeza
Akizungumzia sherehe hizo, Spika wa zamani wa
Bunge, Pius Msekwa alisema kudumu kwa Muungano ni suala la kujivunia
kwani yapo mataifa mengine yaliyoshindwa.
“Tumepita katika mawimbi makubwa au kero za
Muungano huu. Ingawa tumefanikiwa kuyavuka lakini ukweli ni kwamba
yametuyumbisha sana. Ninaandika kitabu ambacho kinazungumzia historia ya
Muungano tangu tulipouanzisha,” alisema Msekwa.
Alitoa mfano wa mataifa yaliyojaribu kuungana na kushindwa kuwa ni Senegal na Gambia; Malaysia na Singapore.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere,
Joseph Butiku alisisitiza vijana kujitokeza kwa wingi na kushiriki
katika Uchaguzi Mkuu ujao.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian
Lubuva alisema: “Nakumbuka sherehe za Muungano za mwaka 1977 niliteuliwa
kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar na tangu hapo nimekuwa nikiitumikia
Serikali. Ni siku ya kumbukumbu yangu muhimu katika maisha na taaluma
pia,” alisema Jaji Lubuva.
Awali
Kabla ya sherehe hizo kuanza, milango ya Uwanja wa
Uhuru ilifunguliwa saa 12.30 asubuhi na wananchi kutoka maeneo
mbalimbali ya jiji kuanza kuingia. Mpaka inatimu saa 2.00 asubuhi uwanja
huo ulikuwa umejaa na wananchi kulazimika kuingia Uwanja wa Taifa.
Dar/Mikoani. Katika kile kinachoonekana kuendelea kujiimarisha
kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa) vimegawana maeneo mbalimbali nchini vikifanya mikutano
ya hadhara na mafunzo kwa viongozi wake ikiwa ni utekelezaji wa mkakati
wa ushindi.
Ukawa unaundwa na vyama vya Chadema, NLD, NCCR-Mageuzi na CUF.
Chadema kilianza ziara zake mikoani wiki
zilizopita baada ya kuzindua mkakati wake uitwao ‘Hakuna kulala, Hakuna
kula, Mpaka Kieleweke’ nchi nzima wakati timu ya NCCR-Mageuzi ikiweka
kambi mkoani Kigoma kwa kile ilichokiita kuimarisha majimbo ya
kimkakati.
Sanjari na vyama hivyo, CUF tangu juzi kiliingia
katika moja ya ngome zake, mkoani Mtwara pamoja na mipango mengine ya
kiushindi, kinahamasisha wananchi kujitokeza kujiandikisha kupiga kura.
Jitihada za Ukawa kuzunguka mikoani zinakuja ikiwa
ni majuma kadhaa tangu Chama cha Mapinduzi (CCM) kikiongozwa na Katibu
Mkuu wake Abdulrahman Kinana kilipomaliza ziara ya kujiimarisha na
kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2010.
Pia, ziara hizo ziligongana na zile za Chama cha ACT - Wazalendo zilizosababisha Chadema na chama hicho kipya kugongana Butiama.
ACT - Wazalendo kinachoongozwa na Zitto Kabwe
kilihitimisha ziara yake ya kimkakati katika mikoa tisa inayoonekana
kuwa ngome ya CCM, wiki iliyopita wilayani Bariadi, Shinyanga na kuvuna
wanachama zaidi 6,000 katika mikoa hiyo.
NCCR-Mageuzi ipo Kigoma
Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Mosena Nyambabe
alisema jana kuwa Ukawa ina mikakati inayofanana ndani ya vyama vyao ya
kuhakikisha inajiimarisha kisiasa nchi nzima ili ishinde Uchaguzi Mkuu.
Alisema siku 10 zilizopita, timu ya NCCR
ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti - Zanzibar, Haji Hamis Hamad ilianza
ziara Kigoma kuhakikisha majimbo ya mkoa huo yanaendelea kuwa ngome
yake.
“Kigoma nzima ina majimbo yetu ya kimkakati na
Ukawa wameshatukabidhi sasa kilichobaki ni kufanya ‘political
management’ (usimamizi wa kisiasa) katika kiwango kinachotakiwa.
“Katika kikosi hicho, pia wamo Katibu Mwenezi,
David Kafulila, Katibu Mkuu Mstaafu, Samuel Ruhuza na Kamishna wa
Kagera, Peterson Mshenyela na wengineo,” alisema Nyambabe.
Alisema baada ya kumalizika ziara katika mkoa huo viongozi hao
wataelekea Kagera kwa kuanzia majimbo ya Ngara na Nkenge, maeneo ambayo
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe anaendelea kumwaga ‘cheche’.
Kinachoendelea katika ziara hizo ni kama
mashambulizi ya ‘bandika bandua’ na kuzuia mparaganyiko ndani ya vyama
hivyo ambao unaweza kutokea baada ya kuanza kwa mchakato wa kugawana
nafasi za udiwani na ubunge.
Chadema kila kona
Chadema, inayoendelea na utoaji wa mafunzo ya
uongozi bora kwa viongozi wa ngazi zote na makada waliotia nia ya
kugombea na mikakati mingine ya ushindi, viongozi wake wa juu
wametawanyika maeneo tafauti katika kanda zake 10 za kiutendaji.
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbrod Slaa aliyekuwa
Morogoro alieleza kuwa Tanzania kwa sasa inasifika nje ya nchi kwa
uvunjifu wa haki za binadamu.
Akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara kwenye
Uwanja wa Shule ya Msingi Kiwanja cha Ndege, Manispaa ya Morogoro juzi,
Dk Slaa alisema katika kipindi cha miaka mitano, utawala wa Rais Jakaya
Kikwete umekuwa na matukio mengi ya uvunjaji wa haki za binadamu.
Alisema hivi karibuni alikuwa Marekani kwa ziara
maalumu na huko alihojiwa na waandishi wa habari katika kituo kimoja cha
redio juu ya masuala ya utawala bora nchini.
Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Zanzibar), Salum
Mwalimu akiwa mkoani Rukwa alisema CCM imepoteza baraka za Mungu kiasi
cha kushindwa kujua mgombea wake wa urais mpaka sasa, jambo ambalo
halijawahi kutokea katika historia ya chama hicho.
Mwalimu aliyekuwa akizungumza kwenye Ukumbi wa
Libori Mjini Sumbawanga, alisema viongozi wanaotokana na Chadema wapaswa
kuwa tayari kusimamia haki kwa gharama zozote, kukataa rushwa na
kupunguza kero kwa wananchi na kuwaonya wasije wakaufanya utawala wa
Chadema kuwa kama wa CCM ambayo inayumba.
“Tuna miezi mitatu imesalia tuanze kampeni, lakini
mpaka sasa CCM haijamjua mgombea wake, lini imewahi kutokea? Mungu
amewachanganya kama wajenzi wa karavati,” alisema Mwalimu ambaye baada
ya mkutano huo aliendelea na ziara yake mjini Makambako, Njombe.
Mwalimu alionyesha kushangazwa na baadhi ya
wafuasi wa Chadema kujiunga na chama cha ACT – Wazalendo na akakiita
kuwa ni chama cha msimu ambacho kitapotea baada ya Uchaguzi Mkuu.
Akiendelea na ziara yake mkoani Kagera, Mbowe
alisema kusuasua kwa uandikishaji wa wapigakura ni kiashiria cha
uvunjifu wa amani inayotokana na hofu ya CCM kuangushwa Oktoba.
Akiwahutubia wakazi wa Mji wa Bukoba juzi katika Uwanja wa
Uhuru, Mbowe alisema nchi inaweza kuingia katika machafuko endapo
litakuwapo jaribio lolote la kuahirisha Uchaguzi Mkuu kama upigaji kura
wa Katiba Inayopendekezwa ulivyoahirishwa.
Alisema uchaguzi siyo suala la dharura na kila
hatua inatakiwa kuwekwa wazi ili kuondoa hofu iliyoanza kujengeka
kutokana na kubakia miezi michache kabla ya Uchaguzi Mkuu.
Profesa Lipumba, Mtwara
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amesema
kuwa endapo Wapinzani wataingia madarakani, kazi ya kwanza
itakayofanyika ni kufumua mikataba yote iliyoingiwa bila kufuata
taratibu.
Alisema asilimia kubwa ya mikataba iliyoingiwa na
Serikali, haiwanufaishi Watanzania walio wengi na zaidi ya hapo haina
tija kwa Taifa.
“Haiwezekani Watanzania wakaishi katika hali ya
umaskini wakati wana rasilimali nzuri, zinazowafanya wafaidi matunda ya
nchi yao, lakini kuna wajanja wachache wanaingia mikataba isiyo na tija,
sasa tukiingia madarakani, tutaifumua,” alisema Profesa Lipumba ambaye
leo atakuwa Kijiji cha Msimbati.
Juzi, akiwa katika Mji wa Mikindani mkoani Mtwara
aliionya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuacha kushughulikia suala la
Kura ya Maoni ya Katiba Inayopendekezwa na badala yake ijikite kuandaa
mazingira ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu ili kulinusuru Taifa kuingia
katika mgogoro usio wa lazima.
Profesa Lipumba alisema NEC isipoteze rasilimali za Taifa na muda kwa jambo lisilo na tija kwa wakati huu.
“Jaji Lubuva (Damian, Mwenyekiti wa NEC)
asiliingize Taifa katika mgogoro, ana haraka gani na Katiba
Inayopendekezwa wakati hili la uandikishaji katika Daftari la Kudumu la
Wapigakura hajalimaliza...? Ashughulikie hili la daftari ndiyo kazi yake
kwa sasa, siyo Katiba,” alisema Profesa Lipumba huku akishangiliwa na
wananchi.
Ukerewe. Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) kimeweka
mkakati utakaowafanya makada wake wavamie majimbo yanayoshikiliwa mapema
na CCM, huku wakichelea kuingia kwenye majimbo yaliyo chini ya chama
hicho kikuu cha upinzani.
Mkakati huo ulitangazwa jana na Mwenyekiti wa
Chadema, Freeman Mbowe wakati akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika
kwenye Uwanja wa Mongella mjini hapa, mkutano ambao ulifurika maelfu ya
watu.
Mbowe alitangaza kupiga marufuku wanachama wa
Chadema kuanza kutangaza nia kwenye majimbo ambayo wenzao wanayashikilia
hadi hapo Bunge la Jamhuri ya Muungano litakapovunjwa.
Lakini alisema wanachama wa Chadema wanaruhusiwa
kuanza purukushani kwenye majimbo ambayo yanashikilia na vyama vingine
hasa chama tawala cha CCM ambacho kinashikilia majimbo mengi.
“Naomba ifahamike Chadema ni zaidi ya ubunge,
tunahitaji amani na siyo kuharibu chama. Chadema itasimamisha watu
makini kwenye maeneo yote katika uchaguzi huu,” alisema mwenyekiti huyo
ambaye yuko kwenye ziara ya mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Mbowe ambaye hakugusia suala la Ukawa katika
mkutano huo, alisema kuwa utaratibu utaandaliwa wa kupata wagombea na
kwamba hata waliokuwa wabunge, wasijihakikishie kuwa watapitishwa tena
kwenye maeneo yao wanayoyaongoza sasa.
“Tutakuja na utaratibu mwingine. Hata wabunge wa
Chadema waliokuwa katika maeneo hayo, wasidhani kwamba watabakia hapo.
Tutasimamisha mtu anayekubalika na watu wote, na utaratibu ukiwekwa,
hata aliyekuwa mbunge anaweza kuondolewa,” alisema Mbowe.
Alisema kuwa Chadema inaamini kuwa katika kila eneo kuna mtu wake ambaye ni makini na ni wazi atashinda.
Vyama vinne vya upinzani, Chadema, NLD,
NCCR-Mageuzi na CUF vimekubaliana kusimamisha mgombea mmoja kuanzia
kwenye uchaguzi wa madiwani hadi rais. Vyama hivyo, vilivyo chini ya
mwavuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), vimekubaliana kuwa kila
chama kipate mgombea wake na baadaye vitachambua anayekubalika na wengi.
Ainanga Nec
Akizungumzia mwenendo wa uboreshaji wa Daftari la
Wapigakura, Mbowe alisema Taifa kwa sasa liko kwenye giza nene kutokana
na maandalizi mabovu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi(Nec).
Mbowe alisema kucheleweshwa kwa kazi ya
uandikishaji wapigakura ni sehemu ya njama za CCM kupitia Serikali yake
inayotamani kutumia nafasi hiyo ili kuendelea na hujuma katika Uchaguzi
Mkuu wa Oktoba.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh.
Lazaro Nyalandu akizungumza katika mkutano uliohusisha wadau wa
mashirika ya Kimataifa na asasi za kijamii ukiwa na lengo la
ushirikishaji wa jamii katika masuala ya uhifadhi wa wanyamapori
uliofanyika jana katika ukumbi wa mikutano wa Mpingo House uliopo Wizara
ya Maliasili na Utalii jijini Dar es Salaam.
Waziri Nyalandu akiendelea kutoa ufafanuzi.
Waziri Nyalandu akikazia jambo.
Naibu Waziri wa Maliaisli na
Utalii, Mahmoud Mgimwa akitoa salamu kwa wadau wa taasisi za kirai.
Kushoto Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Lazaro Nyalandu.
Mratibu wa Uhakiki wa Ubora kutoka
Haki Elimu, Robert Mihayo akitoa maoni kwa Waziri Mh. Nyalandu ambapo
amemuomba kushirikisha wadau wa elimu katika kutoa elimu ya uhifadhi wa
wanyamapori kuanzia ngazi ya elimu ya msingi ili kuwaanda vijana ambao
ni taifa la kesho.
Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation
for Civil Society, Francis Kiwanga akishiriki kutoa maoni katika masuala
ya uhifadhi wa wanyamapori pamoja na kutokemeza ujangili wa Tembo.
WAZIRI wa
Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu amesema kama watanzania
wasiposhirikiana katika kudhibiti ujangili wa Tembo waliopo watatoweka
kabisa katika kipindi cha miaka 10 ijayo.
Kauli hiyo
ameitoa jana kwenye mkutano wa ushirikishwaji wa jamii katika masuala ya
uhifadhi wa wanyamapori uliofanyika wizarani kwake.
“Uhifadhi kama tunavyoujua, hautaweza kufanikiwa kama kila mtu kwenye nchi hii atafikiria ni kazi ya serikali kuu peke yake.
Na vilevile kama kila mtu atafikiria ni kazi ya wahifadhi peke yao”. alisema Nyalandu kwenye mkutano huo.
Nyalandu
alibainisha kuwa, majadiliano hayo, yatakuwa chachu kubwa ya maendeleo
katika wizara hiyo huku akiwashukuru wadau hao mbalimbali wakiwemo
wanahabari kwa kufika kwao, ili kuangalia suala la uhifadhi kwa mapana
yake.
Alisema
wakati ujangili wa Tembo nchini umeshamiri sana, wakati umefika kwa
watanzania kuhakikisha kwamba wanakomesha hali hiyo ili taifa kuendelea
kuwa na wanyama wake.
Alisema
mathalani Tembo katika hifadhi ya Selous wamepungua kutoka Tembo 38,975
katika sensa ya mwaka 2009 hadi Tembo 1,384 kwa sensa ya mwaka 2014 na
akasema kwa kasi hiyo katika miaka 10 ijayo Tembo Tanzania wataisha
kabisa.
“Hili ni
muhimu watu wakafahamu, upana wa hivi vita ni mkubwa kiasi gani na watu
wanaohusika ni wengi kiasi gani ndani na nje ya nchi," alisema Nyalandu
akiongeza kuwa mitandao ya kihalifu imetanda ulimwenguni kote.
Alisema suala la hifadhi halipo kwa wanyama pekee bali lipo katika upana wote na hata katika misitu.
Alisema ili
kukabiliana na ukatwaji hovyo wa miti kutoka katika misitu ya miombo
wanajipanga kuhakikisha kwamba miombo inayodaiwa kuingizwa nchini kutoka
Zambia inakamatwa ili kulinda miombo iliyopo magharibi ya nchi.
Akizungumzia
suala la mifugo na mbuga zinazopakana nazo amesema kwamba wanaanda
rasimu ya kuhakikisha kwamba kuna mahusiano mazuri kati ya wenye mifugo
na hifadhi wakiwa tayari kuyaachia baadhi ya maeneo kwa lengo la
kuhakikisha kwamba wafugaji hawaingizi mifugo yao katika hifadhi.
Aidha amesema
kwamba wanajipanga namna ya kuhakikisha kwamba hakuna mgongano wa
maeneo kati ya wanyama na binadamu na kwamba wanavijiji wanafundishwa
namna ya kuishi na wanyama katika maeneo yenye mwingiliano mkubwa.
Aidha alisema
kwamba meno ya Tembo kilo 1,763 yalikamatwa mwaka jana na jitihada
zinaendelea za kukabiliana na majangili kwa kutanua mtandao wa
kiintelejensia ndani na nje.
Alisema kwa
sasa wanamsaka raia wa China anayeshutumiwa kutorosha nyara za serikali
kwa kushirikiana na jeshi la Polisi la Kimataifa (Interpol).
Kwa nje ya nchi, meno ya Tembo yaliyokamatwa, Kilo 40 katika miji ya Hong Kong, China.
Aidha alisema
watuhumiwa 1,711, walikamatwa kuanzia Januari hadi Desemba mwaka jana
na kesi zao zinaendelea katika mahakama mbalimbali hapa nchini. Pia
silaha 85 zimekamatwa ikiwemo silaha za kivita ambazo walikuwa
wakizitumia mbugani.
Alisema ukichanganya na silaha zilizokamatwa kwenye operesheni tokomeza, jumla silaha 1,199 zimekamatwa.
Kwa upande
wake, Ali Said Mosee aliyehudhuria mkutano huo kutoka Tanzania
Association on Climate Change, alishauri ushirikishaji wa wadau
mbalimbali kutatua migogoro kwenye mipaka ya mbuga na pia mgongano wa
kimaslahi kati ya hifadhi na wanadamu.
Aidha wadau
walishauri Wizara kuhakikisha inapunguza misafara ya wanyama ya
kuhamahama kutoka sehemu moja hadi nyingine ikiwemo kwa kuzalisha miti
na mazao yanayopendwa na wanyama hao.
“Wanyama wetu
wanatakiwa wafanyiwe utafiti na kujua nini Nyati anapendelea kula
porini, basi wapande hiyo miti na vyakula vyake kwa ujumla hata kwa
Tembo hivyo hivyo.Wapande hiyo miti hapa hapa kwani hata siye binadamu
tunavyovyakula tunavyovipenda, naamini hata kwa wanyama ni hivyo hivyo,
rai yangu ni kuwa tufanye utafiti na kujua ili kuzuia misafara hii”
alisema Ali Said Mosee.
Tanzania
inahifadhi za taifa 16 na asilimia 40 ya ardhi ya nchi ni maeneo
yaliyohifadhiwa. Kati ya maeneo hayo yaliyohifadhiwa hadi mwezi uliopita
mwaka huu 2015, maeneo 19 yanamilikiwa na wananchi na yameshasajiliwa.
Pia alisema kwamba kuna mapori ya akiba, 28 nchi nzima.
“Watu wengi
wanadhani kwamba misitu yote inamilikiwa na serikali kuu. Ukweli ni
kwamba serikali kuu inamiliki asilimia 35 tu ya misitu ya nchi yetu,
misitu mingine yote inamilikiwa na vijiji, wilaya na watu binafsi
asilimia 7. " alibainisha waziri huyo.
Aliwataka
watendaji wa Serikali za mitaa kukabiliana na changamoto ya kutoweka kwa
kasi kwa misitu ili taifa lisitumbukie katika jangwa.