KABANG! Baada ya kutoonekana katika pozi za kimahaba
kwa muda mrefu, kwa mara ya kwanza, staa wa sinema za Kibongo,
Jacqueline Wolper Massawe ‘Gambe’ amenaswa ‘live’ na mwanaume anayedaiwa
kuwa ni mume wa mtu, Risasi Jumamosi limesheheni.
Jacqueline Wolper Massawe ‘Gambe’ amenaswa ‘live’ na mwanaume anayedaiwa kuwa ni mume wa mtu.
Kwa muda mrefu Wolper amekuwa makini na picha zake za kimahaba tangu
alipokuwa akitoka kimapenzi na mfanyabiashara maarufu jijini Dar,
Abdallah Mtoro ‘Dallas’.
CHANZO CHAMWAGA MTONYO
Awali, chanzo makini
kilipenyeza habari kuwa kuna mawasiliano yamenaswa ‘kimafia’ ambayo
yalitoka kwa Wolper kwenda kwa rafiki yake yakionesha anabanjuka na
mwanaume huyo wa mtu aliyejulikana kwa jina moja la Gee.
YADAIWA NI MUME WA SHOSTI YAKE
Chanzo hicho
kilikwenda mbali zaidi kwa kudai kwamba licha ya kuwa ni mume wa mtu,
mwanaume huyo ni bwana wa rafiki yake kutokana na mawasiliano hayo
yalivyosomeka.
“Mashabiki kila siku huwa wanamtetea Wolper na skendo zake, sasa
nakutumia picha pamoja na ‘chating’ zake alizokuwa akichati na shoga
yake kuhusiana na jamaa huyo,” kilisema chanzo hicho.
PICHA ZATUA RISASI JUMAMOSI
Baada ya kuzinyaka
habari hizo, mwanahabari wa Risasi Jumamosi alimtafuta sosi huyo na
kufanikiwa kuzitia kibindoni picha hizo kisha kazi ya kuwasaka wahusika
ikaanza.
Wa kwanza kutafutwa alikuwa ni Gee ambaye kwa mujibu wa vyazo
tofauti, ilidaiwa kuwa kwa sasa hayupo Bongo na hakuacha mawasiliano
yoyote tangu alipoondoka.
WOLPER SASA!
Baada ya jitihada za kumsaka mwanaume huyo kugonga mwamba, paparazi wetu alimtwangia simu Wolper ambaye alieleza kila kitu:
Paparazi: Mambo vipi Wolper, nasikia makelele unaweza kusogea sehemu yenye utulivu kuna ishu nataka tuongee?
Wolper: Niko msibani na sasa hivi ndiyo zoezi la kuaga mwili, ngoja niingie kwenye gari nikupigie.
Baada ya dakika 45
Wolper: Haya niambie wangu niko sehemu nzuri.
Paparazi: Ni hivi, kuna habari imetufikia ikiambatanishwa na picha na baadhi ya chating inakuhusu wewe!
Wolper: Habari gani hiyo mbona unanitisha?
Paparazi: Kuna picha zinakuonesha wewe ukiwa katika
pozi la kimalavidavi na jamaa anayedaiwa kuwa ni mume wa mtu. Ukiachana
na picha hizo, zimeambatanishwa chating zinazoonesha ulikuwa ukichati na
rafiki yako kumueleza kuwa mwanaume uliye naye ni mume wa mtu!
Wolper: Kiukweli kabisa bila ya hata kupepesa macho
hizo picha ni zangu na zimepigwa kwa kutumia simu yangu tangu mwaka juzi
lakini kuhusiana na hizo chating siyo zangu hata wewe unaweza kuwa
shahidi kwani mara nyingi huwa tunachati na unajua vizuri ‘floo’ yangu
katika kuandika SMS.
Paparazi: Ok, sawa, lakini turudi katika suala la picha, huyu ndiyo bwana’ko wa sasa?
Wolper:
Hapana, huyo ni mshikaji wangu tu na tulipiga picha hizo tukiwa baa
tena kipindi kile nahamia tu Mwananyamala (Dar) na sasa hivi hata sijui
huyo mshikaji yuko wapi.
Paparazi: Ina maana huna mawasiliano naye kwa muda mrefu, mtu ambaye mlipiga naye picha kimahaba namna hii?
Wolper: Kweli kabisa, sina mawasiliano naye kitambo nikimaliza tu kuongea na wewe nitamtafuta na kumuuliza kulikoni picha hizo kuvuja.
Paparazi: Si ulisema umepiga katika simu yako wewe si ndiyo wa kujiuliza kwa nini picha zimevuja?
Wolper: Nilimzawadia simu kama rafiki yangu na picha zikiwa humohumo sikuzifuta.
Paparazi: Haya Wolper ngoja nikuache mi niendelee na majukumu.
Wolper: Poa wangu baadaye nitakucheki.
WOLPER HUYUHUYU
Hii ni mara ya pili kwa Wolper
kutuhumiwa kukwapua bwana wa rafiki yake. Hivi karibuni mshiriki wa Miss
Tanzania 2012, Husna Maulid alilalamika kuwa Wolper kamchukulia
bwana’ke aliyemtaja kwa jina moja la Rajab, raia wa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo.
Si Wolper pekee, ‘trendi’ inaonesha kuwa mastaa wengi wa kike hasa wa
filamu wamefanya ishu ya kuporana wanaume kuwa sehemu ya utamaduni
katika tasnia hiyo bila kujua wanajiondolea heshima mbele ya jamii.
GPL
No comments:
Post a Comment