Waziri Nyalandu akiendelea kutoa ufafanuzi.
Waziri Nyalandu akikazia jambo.
Naibu Waziri wa Maliaisli na Utalii, Mahmoud Mgimwa akitoa salamu kwa wadau wa taasisi za kirai. Kushoto Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Lazaro Nyalandu.
Mratibu wa Uhakiki wa Ubora kutoka Haki Elimu, Robert Mihayo akitoa maoni kwa Waziri Mh. Nyalandu ambapo amemuomba kushirikisha wadau wa elimu katika kutoa elimu ya uhifadhi wa wanyamapori kuanzia ngazi ya elimu ya msingi ili kuwaanda vijana ambao ni taifa la kesho.
Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation for Civil Society, Francis Kiwanga akishiriki kutoa maoni katika masuala ya uhifadhi wa wanyamapori pamoja na kutokemeza ujangili wa Tembo.
WAZIRI wa
Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu amesema kama watanzania
wasiposhirikiana katika kudhibiti ujangili wa Tembo waliopo watatoweka
kabisa katika kipindi cha miaka 10 ijayo.
Kauli hiyo
ameitoa jana kwenye mkutano wa ushirikishwaji wa jamii katika masuala ya
uhifadhi wa wanyamapori uliofanyika wizarani kwake.
“Uhifadhi kama tunavyoujua, hautaweza kufanikiwa kama kila mtu kwenye nchi hii atafikiria ni kazi ya serikali kuu peke yake.
Na vilevile kama kila mtu atafikiria ni kazi ya wahifadhi peke yao”. alisema Nyalandu kwenye mkutano huo.
Nyalandu
alibainisha kuwa, majadiliano hayo, yatakuwa chachu kubwa ya maendeleo
katika wizara hiyo huku akiwashukuru wadau hao mbalimbali wakiwemo
wanahabari kwa kufika kwao, ili kuangalia suala la uhifadhi kwa mapana
yake.
Alisema
wakati ujangili wa Tembo nchini umeshamiri sana, wakati umefika kwa
watanzania kuhakikisha kwamba wanakomesha hali hiyo ili taifa kuendelea
kuwa na wanyama wake.
Alisema
mathalani Tembo katika hifadhi ya Selous wamepungua kutoka Tembo 38,975
katika sensa ya mwaka 2009 hadi Tembo 1,384 kwa sensa ya mwaka 2014 na
akasema kwa kasi hiyo katika miaka 10 ijayo Tembo Tanzania wataisha
kabisa.
“Hili ni
muhimu watu wakafahamu, upana wa hivi vita ni mkubwa kiasi gani na watu
wanaohusika ni wengi kiasi gani ndani na nje ya nchi," alisema Nyalandu
akiongeza kuwa mitandao ya kihalifu imetanda ulimwenguni kote.
Alisema suala la hifadhi halipo kwa wanyama pekee bali lipo katika upana wote na hata katika misitu.
Alisema ili
kukabiliana na ukatwaji hovyo wa miti kutoka katika misitu ya miombo
wanajipanga kuhakikisha kwamba miombo inayodaiwa kuingizwa nchini kutoka
Zambia inakamatwa ili kulinda miombo iliyopo magharibi ya nchi.
Akizungumzia
suala la mifugo na mbuga zinazopakana nazo amesema kwamba wanaanda
rasimu ya kuhakikisha kwamba kuna mahusiano mazuri kati ya wenye mifugo
na hifadhi wakiwa tayari kuyaachia baadhi ya maeneo kwa lengo la
kuhakikisha kwamba wafugaji hawaingizi mifugo yao katika hifadhi.
Aidha amesema
kwamba wanajipanga namna ya kuhakikisha kwamba hakuna mgongano wa
maeneo kati ya wanyama na binadamu na kwamba wanavijiji wanafundishwa
namna ya kuishi na wanyama katika maeneo yenye mwingiliano mkubwa.
Aidha alisema
kwamba meno ya Tembo kilo 1,763 yalikamatwa mwaka jana na jitihada
zinaendelea za kukabiliana na majangili kwa kutanua mtandao wa
kiintelejensia ndani na nje.
Alisema kwa
sasa wanamsaka raia wa China anayeshutumiwa kutorosha nyara za serikali
kwa kushirikiana na jeshi la Polisi la Kimataifa (Interpol).
Kwa nje ya nchi, meno ya Tembo yaliyokamatwa, Kilo 40 katika miji ya Hong Kong, China.
Aidha alisema
watuhumiwa 1,711, walikamatwa kuanzia Januari hadi Desemba mwaka jana
na kesi zao zinaendelea katika mahakama mbalimbali hapa nchini. Pia
silaha 85 zimekamatwa ikiwemo silaha za kivita ambazo walikuwa
wakizitumia mbugani.
Alisema ukichanganya na silaha zilizokamatwa kwenye operesheni tokomeza, jumla silaha 1,199 zimekamatwa.
Kwa upande
wake, Ali Said Mosee aliyehudhuria mkutano huo kutoka Tanzania
Association on Climate Change, alishauri ushirikishaji wa wadau
mbalimbali kutatua migogoro kwenye mipaka ya mbuga na pia mgongano wa
kimaslahi kati ya hifadhi na wanadamu.
Aidha wadau
walishauri Wizara kuhakikisha inapunguza misafara ya wanyama ya
kuhamahama kutoka sehemu moja hadi nyingine ikiwemo kwa kuzalisha miti
na mazao yanayopendwa na wanyama hao.
“Wanyama wetu
wanatakiwa wafanyiwe utafiti na kujua nini Nyati anapendelea kula
porini, basi wapande hiyo miti na vyakula vyake kwa ujumla hata kwa
Tembo hivyo hivyo.Wapande hiyo miti hapa hapa kwani hata siye binadamu
tunavyovyakula tunavyovipenda, naamini hata kwa wanyama ni hivyo hivyo,
rai yangu ni kuwa tufanye utafiti na kujua ili kuzuia misafara hii”
alisema Ali Said Mosee.
Tanzania
inahifadhi za taifa 16 na asilimia 40 ya ardhi ya nchi ni maeneo
yaliyohifadhiwa. Kati ya maeneo hayo yaliyohifadhiwa hadi mwezi uliopita
mwaka huu 2015, maeneo 19 yanamilikiwa na wananchi na yameshasajiliwa.
Pia alisema kwamba kuna mapori ya akiba, 28 nchi nzima.
“Watu wengi
wanadhani kwamba misitu yote inamilikiwa na serikali kuu. Ukweli ni
kwamba serikali kuu inamiliki asilimia 35 tu ya misitu ya nchi yetu,
misitu mingine yote inamilikiwa na vijiji, wilaya na watu binafsi
asilimia 7. " alibainisha waziri huyo.
Aliwataka
watendaji wa Serikali za mitaa kukabiliana na changamoto ya kutoweka kwa
kasi kwa misitu ili taifa lisitumbukie katika jangwa.
No comments:
Post a Comment