Thursday, September 11, 2014

UCHAGUZI CHADEMA: HAWA HAPA VIONGOZI WAPYA WA BAVICHA.

Mwenyekiti mpya wa BAVICHA, Paschal Patrobas Katambi

Makamu Mwenyekiti, Patrick Ole Sosopi

Chama cha Demokrasia na maendelea kimepata viongozi wake wapya wa baraza la vijana chadema (BAVICHA),Mwenyekiti wa baraza hilo la vijana ni Paschal Patrobasi Katambi na makamu mwenyekiti ni Ptrick Patrick Ole Sosopi,katika uchaguzi huo uliokuwa wenye ushindani mkubwa hasa kwa nafasi ya mwenyekiti na makamu mwenyekiti wa BAVICHA hali iliyowapa wakati mgumu watabiri kubashiri nani angeibuka na ushindi katika nafasi hizo nyeti kabisa,mchuano huo mkali huo ulitokana na vijana wengi wenye uwezo na sifa kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi hizo muhimu hali iliyopelekea ushindani kuwa kuwa mkali sana.

Kutokana na ushindani mkali uliokuwepo ililazimu uchaguzi wa mwenyekiti na makamu mwenyekiti uingie hatua ya pili (round ya pili) kutokana na matokeo ya awali kushindwa kutoa mshindi alievuka asilimia 50%,

Wagombea walioingia nafasi ya pili kwa nafasi ya mwenyekiti walikuwa Patrobasi na mwanadada pekee aliejitokeza kugombea nafasi hiyo Upendo Peneza,na kwa upande wa makamu mwenyekiti walikuwa ni Ole Sosopi na Jesca Kishoa,katika awamu hiyo ya pili,Patrobasi aliibuka mshindi katika nafasi ya mwenyekiti kwa kupata jumla ya kura 173 na kwa upande wa makamu mwenyekiti Sosopi alifanikiwa kuibuka mshindi kwa idadi ya kura 128.
Zeudi Abdalah amefanikiwa kuwa makamu mwenyekiti kwa upande wa Zanzibar kwa kupata idadi ya kura 157,hivyo atakuwa ni makamu mwenyekiti kutoka zanzibar katika kipindi cha miaka 5

Awali uchaguzi huo uliokuwa umetangazwa kurushwa moja kwa moja na kituo cha ITV na baadae kushindikana ,ulikuwa ukifatiliwa na mamilioni ya watanzania wa rika zote kutoka mikoa yote,na ulilazimika kuisha usiku sana wa majira ya saa 11 kasoro kutokana na taratibu za uchaguzi na idadi kubwa ya wagombea kwenye kila nafasi.
Wagombea wengine wenye nguv BAVICHA walikuwa Philip Philipo Mwakibinga,Daniel Daniel Naftal na wengineo.,mwenyekiti huyo mpya alishawahi kuwa mwenyekiti wa CHASO SAUT Mwanza mwaka 2011-2012 na makamu wake anatokea Iringa ..
Leo ni zamu ya wanawake kupimana nguvu katika nafasi mbalimbali ,ni katika mwendelezo wa ratiba ya chaguzi ndani ya CHADEMA,safari itakayohitimishwa kwa kumchagua mwenyekiti wa chama taifa

No comments:

Post a Comment