Maafisa wa usalama wa Nigeria wamesema kuwa zaidi ya wanawake 60 wakiwemo wasichana wa umri mdogo wamekewpa kutoka kwa wanamgambo wa Boko Haram waliokuwa wamewateka nyara.
Wanawake hao wanaaminiwa kuwa miongoni mwa wanawake 68 waliotekwa mwezi uliopita karibu na mji wa Damboa kaskazni mashariki mwa jimbo la Borno.serikali ya Nigeria imeitisha kufanywe uchunguzi wa kina juu ya namna walivyotoweka wasichana hao.
wapiganaji wa Boko Haram
Baadhi ya vyombo vya habari nchini humo vinadai kuwa huenda wasichana hao walitoroka siku ya Ijumaa, pale watekaji nyara walipokwenda kushamblia kambi ya kijeshi. Msemaji wa jeshi la Nigeria amesema kuwa Ijumaa hiyo (4 Julai) walifanikiwa kuwaua wapiganaji zaidi ya 50 karibu na mji wa Damboa.
Bado wasichana wengine hawajapatikana
Hata hivyo bado wanamgambo hao wa Boko Haram wanawazuilia zaidi ya wasichana wengine 200 waliowateka nyara mwezi Aprili. Hatua ambayo imekemewa vikali na jamii ya kimataifa huku baadhi ya mataifa kama vile Marekani, Uingereza na hata Ufaransa wakijitolea kuisaidia serikali ya Nigeria kuwasaka wasichana hao.BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment