JAMBO limezua jambo! Yule jamaa aliyefahamika kwa jina la Huruma Bernard
ambaye alidai kumfumania baba mwenye nyumba wake, Lugali akitaka
kuvunja amri ya sita na mkewe, hatimaye ameamua kuhama nyumba.
...Hivi ndivyo ilivyokuwa wakati wa fumanizi.
Fumanizi hilo liliripotiwa na gazeti hili, toleo la wiki iliyopita
likiwa na kichwa cha habari, ‘VUNJA JUNGU GESTI’ ambapo Huruma
alimfumania baba mwenye nyumba huyo kwenye gesti moja iliyopo Buguruni,
Dar.
Bw. Huruma Bernard ambaye alidai kumfumania baba mwenye nyumba wake, Lugali akihama na mkewe kutoka nyumba waliyopanga.
Katika tukio la kuhama, Ijumaa iliyopita, wanahabari wetu walitonywa na
chanzo chao kuwa Huruma alikuwa anahama katika nyumba aliyokuwa anaishi
maeneo ya Ukonga, Dar baada ya kupewa notisi na baba mwenye nyumba huyo
ili kuondoa fedheha ya kumfumania gesti na mkewe.
...Mke na mume walifunga virago vyote tayari kwa kuhama.
Wanahabari wetu walipofika eneo hilo walimkuta Huruma na mkewe wakibeba
vitu ambapo jamaa huyo alisema kuwa amekubali kuondoka kwenye nyumba
hiyo baada ya kuona hakutakuwa na maelewano tena.
...Mke na mume wakiwa nje ya nyumba waliyopanga.
“Nimekubali kuhama kwani maelewano na baba mwenye nyumba hayakuwa mazuri
tena baada ya kumfumania na mke wangu,” alisema Huruma.
...Mke na mume hao wakiondoka.
Alisema kwamba mkataba wake katika nyumba hiyo ulikuwa unatakiwa
umalizike Machi Mosi, mwakani lakini baada ya kumfumania wamekuwa na
bifu kubwa kiasi cha kukaribia kutwangana kila wanapopishana.
Shauri lao bado lipo kwenye Kituo cha Polisi cha Buguruni likiwa na
faili la kesi namba BUG/RB/6182/ 2014- UTEKAJI kwani baada ya fumanizi
jamaa huyo alidai alitekwa.
No comments:
Post a Comment