Wednesday, July 2, 2014

TOHARA YA PORINI YAWAUA VIJANA 19 AFRIKA KUSINI


Wizara ya Afya nchini Afrika Kusini inasema kuwa wavulana kumi na tisa wameaga dunia mwaka huu katika sherehe za kitamaduni za kuwapasha tohara wavulana.
Tohara hiyo ni utamaduni unaopewa heshima kubwa katika baadhi ya maeneo ya taifa hilo.
Utamaduni wa tohara ni muhimu kwa vijana hasa kwa kuwa ni njia ya vijana kuingia utu uzima, lakini baadhi hufariki wakipitia utamaduni huo na wengine hupoteza sehemu zao nyeti.
Vijana 19 wamefariki kufika sasa na wengine 50 wako hospitalini.
Wanapokea matibabu ya kukosa maji mwilini, sehemu zao za siri kuoza na majerahe mengine mabaya.
Wazee wa kijamii wasiokuwa na mafunzo ya kufanya tohara ambao huendesha vituo vya kuwapasha tohara vijana wamelaumiwa kwa vifo kama hivyo.
Katika baadhi ya visa ambavyo vimeripotiwa, vijana hutoroka na kujiunga na vijana wengine wanaokwenda katika vituo hivyo haramu bila ya idhini ya wazazi.
Serikali imewasihi wazee wa kijamii kushirikiana na watu wenye uwezo wa kitaalamu na madaktari ili kuwapasha tohara vijana na kuzuia vifo.
Mwezi jana watu 23 walikamatwa kwa vifo vya vijana waliofariki kutokana na athari za kupashwa toihara.

BBC SWAHILI

No comments:

Post a Comment