Mtuhumiwa wa kesi ya kumtesa hausigeli wake, Yasinta Rwechengura baada ya kushuka kutoka kwenye gari la magereza akielekea kizimbani chizi ya ulinzi mkali wa askari magereza.
Ndugu wa Yasinta wakiwa nje ya jengo la Mahakama ya Kinondoni kabla ya mtuhumiwa huyo kupandishwa kizimbani.…
Mtuhumiwa wa Kesi ya jinai, Yasinta Rwechengura mkazi wa Boko-Magengeni, Dar anayetuhumiwa kwa kumjeruhi mfanyakazi wake wa ndani aitwaye Melina Mathayo (15) kwa kumpiga na nyaya za Kompyuta na kwanja la kuzolea majani maarufu kama leki na kumsababishia majeraha makubwa kichwani na sehemu nyingine za mwili ameendelea kusota rumande.
Tukio hilo la kikatili lilitokea mapema Juni 11, mwaka huu majira ya saa 3 usiku maeneo ya Boko, nje kidogo ya Dar baada ya mwenye nyumba huyo kufanya kitendo hicho kwa madai ya kuwa mfanyakazi wake huyo alikuwa kiburi kila alipomtuma kazi za ndani.
Akisoma shitaka hilo, Wakili wa Serikali, Credo Lugaju mbele ya Hakimu Mkazi Boniphace Lihamwike alisema kuwa kesi hiyo imeahirishwa kutokana na hudhuru mbalimbali uliojitokeza kwa Hakimu wa awali aliyepangiwa kesi hiyo.
Kesi hiyo itasikilizwa tena Julai 11 mwaka huu baada ya kupangiwa hakimu mpya na mtuhumiwa kurudishwa rumande
No comments:
Post a Comment