Tuesday, July 22, 2014
MSHTUKO DAR: VIUNGO VINGI VYA BINADAMU VYANASWA BUNJU, DAR
JESHI la Polisi Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam usiku wa Julai 21, mwaka huu limekamata viungo mbalimbali vya binadamu vilivyowekwa kwenye mifuko ya plastiki na kuhifadhiwa katika machimbo ya kokoto ya Bunju nje kidogo ya jiji la Dar es salaam. Mpaka sasa bado haijafahamika viungo hivyo vilitoka wapi.
Taarifa za tukio hilo zilithibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Camilius Wambura ambaye leo atatoa taarifa zaidi kuhusu tukio hilo.
Viungo hivyo vilichukuliwa na Jeshi la Polisi kwa uchunguzi zaidi.
Endelea kutembelea tovuti hii kujua nini kinaendelea kuhusu sakata hili.
Labels:
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment