Saturday, July 26, 2014

MKE WA MBUNGE WA CCM ADAIWA KUMUUA HOUSE GIRL WAKE KIKATILI

Mbunge wa Moshi vijijini Cyrill Chami ambaye mkewe anatuhumiwa kumuua mfanyakazi wa ndani kwa kipigo

Mfanyakazi wa ndani wa mbunge wa Jimbo la Moshi vijijini Cyril Chami (CCM) aitwaye Mariam Said (16) amefariki dunia mapema alfajiri ya leo ikiaminika kwabmba kifo chake kimesababishwa na kipigo toka kwa mke wa Mbunge huyo.
Sababu kubwa ikielezwa kuwa binti huyo ambaye ni muislamu alikataa kwenda kuhudhuria misa kanisani siku ya jumapili na amekua na tabia ya kupinga kwenda kanisani kila mara tangu aajiriwe na mbunge huyo kwa madai kuwa ni kinyume na imani yake (Uislamu).
Msimamo wa binti huyo ulimpelekea kipigo kikali usiku wa siku hiyo (jumapili) ambapo inadaiwa alivunjika mbavu baada ya mke wa mbunge kumpiga na stuli ubavuni.
Majirani wa mbunge huyo wanasema licha ya binti huyo kuvunjika mbavu hakupewa matibabu yoyote badala yake alifungiwa ndani huku akiendelea kulazimishwa kufanya kazi.
Mbaya zaidi mke wa Mbunge huyo alimnyang'anya simu binti huyo ili asiweze kuwasiliana na familia yake na kuwaeleza yaliyompata. Hata majirani walipomuuliza juu ya hali ya mtoto huyo aliwajibu kwa lugha ya kejeli na kuwaambia hakuna mtu anaweza kumfanya chochote, kwani serikali ni yao.
Kutokana na maumivu makali pamoja na kukosa matibabu hatimaye binti huyo amefariki dunia leo asubuhi.
Source: Radio Moshi Fm

No comments:

Post a Comment