Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Edward Moringe Sokoine (kulia) enzi za uhai wake akiwa na Mwalimu Nyerere.
WAZIRI Mkuu (sasa ni marehemu) Edward Moringe Sokoine alikuwa Dodoma
kwenye kikao cha Bunge akiwa ni kiongozi wa shughuli za serikali na
alimaliza kikao chake Aprili 11, 1984.
Aliandaliwa usafiri wa ndege ili asafiri na ujumbe wake wakati wa
kurejea Dar es Salaam kuendelea na majukumu mengine ya kitaifa lakini
alikataa.
“Safari hii sitaki kurudi Dar es Salaam kwa ndege, nataka kurudi kwa
gari ili nione hali ya mazao ya wakulima njiani,” alikaririwa afisa
mmoja wa Ikulu akimkariri Waziri Mkuu Sokoine mara baada ya kujulishwa
habari ya usafiri wa kumrejesha Dar.
Aprili 12, 1984 msafara wake ulianza akitokea Dodoma huku ukisindikizwa na magari ya polisi na wana usalama wa taifa.
Msafara wake mchana ulipofika eneo la Wami mkoani Morogoro, jirani na
palipojengwa makao makuu ya sasa ya Wilaya ya Mvomero, gari yake
ilipata ajali kwa kugongwa na gari lingine aina ya Toyota Land Cruiser.
Gari hilo lilikuwa likiendeshwa na mkimbizi, raia wa Afika Kusini
ambaye jina lake ni Dumisani Dube aliyekuwa anaishi kwenye kambi ya
wanachama wa chama cha kupigania uhuru wa nchi hiyo cha African National
Congress (ANC), Dakawa, Morogoro.
Sokoine alipofikishwa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, madaktari walithibitisha kifo chake.
Rais (wa wakati huo), Mwalimu Julius Kambarage Nyerere siku hiyo majira
ya jioni alilitangazia taifa kifo cha waziri mkuu wao. Mwalimu Nyerere,
alishindwa kuhutubia kutokana na majonzi aliyokuwa nayo.
Dumisani alishitakiwa mahakamani lakini kesi yake haikuendelea (bila
shaka kwa sababu za kisiasa), aliachiwa huru lakini alirudishwa kwao
Afrika Kusini.
Miaka kumi baada ya kifo chache, daktari aliyeufanyia uchunguzi mwili
wa Sokoine baada ya kifo, aliweka wazi taarifa ya chanzo cha kifo
chake.
Sehemu ya taarifa hiyo ilisema kuwa baada ya ajali, Sokoine
alivunjika shingo ambayo ilisababisha kubana mishipa ya fahamu (spinal
cord) ambayo ilikata mawasiliano kati ya ubongo na sehemu nyingine za
mwili.
Kabla ya kifo chake, Sokoine alikuwa pia Mbunge wa Jimbo la Monduli
na mwili wake ulizikwa huko kwa heshima zote za kiserikali, japokuwa
mila za Kimasai pia zilipewa nafasi katika mazishi hayo.
Mahali alipopatia ajali Sokoine mara baada ya ajali hiyo panaitwa Wami Sokoine na pamejengwa mnara wa
No comments:
Post a Comment