BEAUTIFUL Onyinye, Wema Isaac Sepetu (25), amemlipua aliyekuwa shosti wake, Kajala Masanja ‘K’ ambaye wiki iliyopita alimwita mnafiki.
Habari hiyo ya kuitwa mnafiki iliandikwa kwenye gazeti hili toleo
lililopita iliyokuwa na kichwa kisemacho; ‘Kajala: Wema mnafiki’.
Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu (25)
Katika habari hiyo, Kajala alikaririwa akisema kwamba licha ya watu
wengi kuamini wamepatana, hakuna ukweli kwani rafiki yake huyo ni
mnafiki kufuatia kutomthamini na kutokuwa karibu naye kama zamani
likiwemo suala la kumsifia mtu ambaye alikuwa na ugomvi na Kajala
(Dacutee).
Akizungumza na gazeti hili nyumbani kwake Kijitonyama
jijini Dar, Wema alisema alishangaa kuona Kajala anamwita mnafiki wakati
hakuwahi kupatana naye tangu walipotofautiana kipindi cha nyuma kama
alivyosema.
Wema Sepetu akiwa na shosti wake mpya, Anti Ezekiel.
“Nashangaa Kajala ananiambia mimi ni mnafiki ‘ok fine’ na huo unafiki
wangu unakuja pale nilipomu-wish Dacutee siku yake ya kuzaliwa,
alitakaje eti? Yaani kwa kuwa yeye ana bifu la kumchukulia bwana’ke na
mimi nijiingize kwenye bifu lao?
“Au tofauti zangu mimi na yeye, Aunty Ezekiel aingilie, itakuwa
sahihi kweli kama wanavyofanya hao watu wake anaozurura nao siku hizi?
Wanaingilia vitu ambavyo hawavijui kiundani wake? Nasema siyo sahihi
kabisa mimi nitabaki kama Wema Sepetu na yeye atabaki kama Kajala
Masanja na asifikirie kuwa nitakuja kuwa kama zamani na yeye halafu kama
anamaindi kuhusiana na Dacutee mbona Petit Man ambaye ana uhusiano naye
aliweka picha ya Dacutee na kumu-wish hajammaindi?” aliwaka Wema.
Akiendelea kutema cheche mbele ya kinasa sauti chetu, Wema alisema
anachopaswa kuzungumza Kajala ni ukweli wa matatizo yao na siyo
kusingizia watu wengine.
Wema Sepetu akiwa na shosti yake, Kajala Masanja.
“Mbona siku ile niliwahadithia kila kitu (waandishi) kuhusiana na
tatizo letu, si nimetoa kinyongo changu ambacho nilikuwa nacho siku
nyingi hivi sasa najiona mwepesi na kama na yeye anataka kusafisha moyo
wake anatakiwa afunguke, kuanzia leo nataka niseme sitaki kusikia na
kuulizwa suala la mimi na Kajala kwani nimechoka na nina mambo mengi ya
kufanya,” alisema Wema.
Akizungumzia ishu ya kukutana na Kajala na kupiga picha za pamoja
wakiserebuka hivi karibuni, Wema alisema alifanya vile kuonesha kwamba
hana kinyongo na ndiyo maana alivyoombwa apige picha na Kajala, hakusita
kufanya hivyo.
“Mimi ni mtoto wa Kiislamu na nina imani na upendo kwa kila mtu,
siwezi nikamkatisha mtu furaha yake na ndivyo ilivyotokea, niliombwa
nipige picha ya pamoja na Kajala siku ile ya shughuli na nilifanya hivyo
baada ya pale nikaenda zangu kulala,” alimalizia kusema Wema.
Bifu la mastaa hao wakali wa Bongo Movies liliibuka baada ya Wema
kumtuhumu Kajala kuwa ametembea na aliyekuwa bwana’ke, kigogo aliyetajwa
kwa jina la CK.
No comments:
Post a Comment