Wednesday, June 11, 2014

WAMBURA ARUKA KIUNZI SIMBA, TFF YAMNASUA.... SASA KUGOMBEA UENYEKITI SIMBA

Shabiki wa Simba akifurahi kwa kuonyesha Katiba ya Simba

 Mashabiki wa Simba wakionesha furaha yao klabuni Mtaa wa Msimbazi, Kariakoo.

 Ilikuwa ni pata-shika nguo-kuchanika na pongezi motomoto kwa shujaa wao Wambura.

 Sherehe za kumpongeza Wambura zikiendelea.

 Chereko za kufa mtu zikiendelea mchana huu.

 SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetupilia mbali pingamizi lililowekwa na wanachama wa Simba na kumruhusu mgombea wa nafasi ya urais katika klabu hiyo, Michael Wambura kuendelea na mchakato huo.
Mwenyikiti wa Kamati ya Rufaa wa TFF, Julius Lugazia alipotangaza rufaa hiyo alisema Wambura ni mwanachama halali wa Klabu ya Simba kisheria hivyo anayo haki ya kugombea nafasi hiyo kama wagombea wengine kwani amekuwa akishirikishwa katika kamati mbalimbali huku mchango wake wa kimawazo ukitumika ndani ya klabu hiyo
Mashabiki wa Klabu ya Simba ambao ni wafuasi wa Wambura, walipokea taarifa hiyo ya TFF kwa mikono miwili na kushangilia kwa staili ya kipekee kwenye makao makuu ya klabu hiyo mtaa wa Msimbazi kwa kufurahishwa na maamuzi hayo.

No comments:

Post a Comment