WAKATI vifo mfululizo vikitokea Mei mwaka huu miongoni
mwa wasanii maarufu nchini, nyota wa filamu Bongo, Devotha Mbaga
ameibuka na kusema endapo ataaga dunia, hahitaji kufanyiwa mbwembwe
wakati wa msiba na mazishi yake kama wasanii wengine walivyofanyiwa.
Msanii maarufu wa filamu Bongo, Devotha Mbaga.
Akistorisha na gazeti hili, Devotha alisema hatahitaji kununuliwa
jeneza la kifahari, bali lichongwe kwa mbao za kawaida na lisiwekwe
mapambo yoyote, watu wasilie msibani kwake na kwamba endapo vitu hivyo
vitakiukwa, basi mwili wake utagoma kubebeka.
“Unajua duniani nimekuja uchi, sasa siku nikifa sitaki mbwembwe za
kununuliwa jeneza la mamilioni wakati nimeacha watoto, ni bora hizo
fedha wapewe wanangu ziwasaidie, vivyo hivyo pia sitaki watu walie kwa
kuomboleza kwenye msiba wangu kwa sababu watakuwa wananiumiza tu, hata
watoto na ndugu zangu nilishawaambia,” alisema Devotha.
Devotha Mbaga (kulia) akiwa katika moja ya misiba ya wasanii wenzake.
Katika misiba ya hivi karibuni ya wasanii nyota, imeshuhudiwa kamati
mbalimbali zikiundwa na kuchangisha fedha nyingi ambazo zimekuwa
zikitumika kununulia majeneza ya bei mbaya, vyakula vya gharama na
shughuli zingine ikiwemo ukodishaji wa magari ya kusindikiza msafara
wakati wa mazishi.
No comments:
Post a Comment