Thursday, June 26, 2014

VIFO MFULULIZO VYA WASANII VYAMBADILI BABY MADAHA

Kufuatia vifo vya wasanii vilivyotokea mfululizo, mwigizaji Baby Joseph Madaha amelazimika kubadili mtindo wake wa maisha na kuishi kitakatifu.

 Staa wa filamu Bongo Baby Joseph Madaha

 Akipiga stori na paparazi wetu,  Baby  Madaha alisema anawasihi hata wasanii wenzake wabadili mfumo wa maisha kwa kumgeukia Mungu na kufanya ibada kila mara kwa kuwa vifo hivyo vinawapa somo la kuwakumbusha kumkaribia Mungu.
“Nimebadili mfumo wa maisha kwa kufanya ibada na ninawashauri wasanii wenzangu  tumgeukie Mungu kwani vifo na mambo yanayotokea yanatukumbusha ibada na kujiweka safi,” alisema Baby Madaha.

No comments:

Post a Comment