UNAWEZA kusema ni majanga juu ya majanga yanazidi
kumkumba modo wa Bongo, Jacqueline Patrick ‘Jack’ baada ya wiki
iliyopita kushindwa kupanda kortini kufuatia kutetereka kwa afya yake
bila kufafanuliwa.
Mbali na kuwa na afya tete, pia Jack anadaiwa kulalamikia haki za
msingi za kibinadamu ambazo anazikosa mahabusu kwa kuishi maisha kama ya
mtu aliye kifungoni.
Akizungumza na Amani juzi jijini Dar, mtu anayejitolea kumpa msaada
na kumtembelea Jack mahabusu, Macau, China alikoshikiliwa, Matilda
alisema Jack anaumia kwa kupewa maisha kama tayari amehukumiwa, anaona
bora hukumu yake ipite ajue moja.
“Kiukweli Jack anaumwa, alishindwa hata kwenda mahamani, mbaya zaidi hata wakili wake naye hakutokea siku hiyo.
“Halafu kule mahabusu anafanyishwa kazi ngumu ambazo hastahili kama
mahabusu na amesema hata watu wake wa karibu ambao anaamini kwa kipindi
hiki wangekuwa wanampa faraja hawaoni, anatamani angekamatiwa Bongo
labda kuna watu wanapenda kwenda kumtembelea kule Macau lakini hawana
uwezo.
“Wabongo wengi ambao wako Macau kwa ajili ya sanaa ya sarakasi ndiyo
kidogo wanakwenda kumtembelea siku mojamoja,” alisema Matilda.
Juni 20, mwaka huu, Amani lilizungumza na Mbongo Fleva anayedaiwa ni
mtu wa karibu na Jack, Juma Khalid ‘Jux’ na kumuuliza kwa nini hajawahi
kwenda kumtembelea ‘bebi’ wake mahabusu kama wanavyofanya Wabongo ambao
wako Macau, akajibu:
“Sipendi kusikia ishu yoyote inayomuhusu Jack kwani nina mambo mengi ya kuongelea na si ishu za Jack kila kukicha.
“Kwa kipindi hiki sitahitaji mtu aniulize ishu za Jack, zinanitibua sana na kama kuongelewa zimeshaongelewa hivyo sioni kipya.”
Hii ni mara ya tatu kwa Jack kupanda mahakamani, mara ya kwanza
ilikuwa Aprili 10, mwaka huu kosa likiwa kukutwa na madawa ya kulevya
tumboni aina ya heroin kete 57 au kilo 1.1 yenye thamani ya zaidi ya
shilingi milioni 223. Mara ya pili ilikuwa Mei 23, mwaka huu.
No comments:
Post a Comment