MACHOZI upya! Habari halali kwa ubongo wako zinaeleza
kwamba wakati mumewe, Emmanuel Mbasha (32) alipokuwa mahabusu, Dar kati
ya Juni 15 hadi 17, mwaka huu, staa wa Gospo Bongo, Flora Mbasha (31)
anadaiwa kwenda nyumbani na kukomba vitu vya ndani kuvipeleka
kusikojulikana.
Sehemu ya chumba cha kupumzikia kilichobakiwa na kochi na zulia.
Ilisemekana kwamba wakati hayo yakiendelea, Mbasha alikuwa nyuma ya
nondo za Mahabusu ya Keko jijini Dar es Salaam ambako alishikiliwa.
Kwa mujibu wa mtu aliyeambatana na Mbasha alipopata dhamana dhidi ya
kesi yake inayomkabili ya ubakaji wa shemejiye mwenye umri wa miaka 17,
alipofika nyumbani kwake Tabata-Kimanga, Dar alipigwa butwaa kukuta
hakuna vitu ndani!
Chumba kingine kilichosafishwa kabisa bila ya samani yoyote.
Habari zilidai kwamba alipowauliza majirani kama walimuona mtu
akiingia ndani walimwambia mkewe (Flora) ndiye alikuwa akiingia na
kutoka mara kwa mara.
Ilielezwa kuwa vitu hivyo vilihamishwa Juni 16 ambapo Mbasha alitoka mahabusu Juni 17, yaani siku moja tu.
KITANDA CHA BEI MBAYA
Baadhi ya vitu
vilivyodaiwa kuchukuliwa nyumbani hapo ni kitanda cha bei mbaya
walichokuwa wakilalia kwenye chumba cha baba na mama huku akimwachia
neti ikiwa inaning’inia.
SUTI ZA MAREKANI
Vingine ni makochi huku akibakisha
sofa ndogo ya mtu mmoja, vitu vyote jikoni na nguo (suti za bei mbaya,
walizonunua wakati wakiwa Marekani).
Pia alidaiwa kukomba vile vidani vyote vya dhahabu.
Mwandishi wa Global Bw. Harun Sanchawa akipata undani wa habari kutoka kwa baba mzazi wa Emmanuel Mbasha, mzee Maneno.
ZAIDI YA MIL. 13
Ukiacha zile hati za nyumba,
viwanja na mashamba, gharama ya vitu vyote vilivyochukuliwa ndani ni
zaidi ya Sh. milioni 13 za Kitanzania (kama zile ambazo Wema Isaac
Sepetu alizomlipia Kajala Masanja asiende jela).
AMWAGA CHOZI
Baada ya kukutana na mazingira ya
aina hiyo, lilikuwa ni pigo lingine zito kwa Mbasha ambaye alijikuta
akimwaga chozi kwa mara nyingine kwa sababu ya mkewe Flora aliyedumu
naye katika ndoa kwa takriban miaka 12.
Ilidaiwa kuwa, Mbasha aliumia kupita kiasi huku akiomba Watanzania waone ubaya aliotendewa.
Bw. Harun Sanchawa akihojiana na mama mzazi wa Emmanuel Mbasha.
AMANI LAPEKUWA CHUMBA HADI CHUMBA
Baada ya
kunyetishiwa ishu hiyo, Amani lilifika nyumbani hapo ambapo lilipata
mwanya wa kuingia ndani ya nyumba hiyo kisha kupekuwa chumba hadi chumba
na kujionea kulivyokuwa kweupe huku madirishani mapazia yakiendelea
kubembea kwa upepo mkali uliopo Dar kwa sasa.
Kimuonekano, nyumba hiyo ilikuwa kama kuna familia ilihama hivyo inahitaji kupangishwa au kuhamiwa na mwingine.
Bw. Emmanuel Mbasha.
MBASHA ANASEMAJE?
Alipotafutwa Mbasha kuzungumzia ishu hiyo alikiri kukuta hali hiyo nyumbani kwake baada ya kupata dhamana.
“Nilipofika nyumbani kwangu nilikuta ufunguo wa nyumba kwa majirani.
Niliwauliza kama kulikuwa na mtu anaingia nyumbani nikaambiwa ni Flora.
Kama mnavyoona kuna vitu vingi vya ndani havipo,” alisema Mbasha.
Alipoulizwa kama ana uhakika kuwa mhusika ni Flora, Mbasha alisema yeye alikuta nyumba nyeupe.
Jitihada za kumpata Flora hazikuzaa matunda kwani simu yake ya
kiganjani haikuwa hewani juzi Jumanne mpaka gazeti hili linakwenda
mitamboni.
Flora Mbasha.
TUMEFIKAJE HAPA?
Kabla ya Mbasha kukabiliwa na
kesi hiyo ya madai ya ubakaji wa ndugu wa Flora, Mei 23 na 25, mwaka
huu, tayari kulikuwa na mgogoro wa ndoa. Flora alishaondoka nyumbani na
kwenda kuishi hotelini maeneo ya Sinza jijini Dar.
NINI KINAENDELEA?
Wakati kesi ya ubakaji
ikiendelea kwenye Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Dar huku Mbasha akiwa nje
kwa dhamana, kuna jitihada zinazoendelea ili warudiane kwani kashfa
hiyo inashusha upako wa huduma yao kwa jamii huku wote wakiwa tayari kwa
suluhu.
No comments:
Post a Comment