Baadhi ya mastaa wote waliyojipatia tuzo wakiwa kwenye pozi la pamoja muda mfupi baada ya zoezi la utoaji tuzo kukamilika.
Miss Tanzania 2004, Faraja Kota (kulia), akimkabidhi tuzo ya Msanii Bora wa Filamu Anayependwa, Mzee Majuto.
Mtangazaji wa kipindi cha
Amplifier, Millard Ayo (kushoto), akipokea tuzo ya Mtangazaji wa Redio
Anayependwa Zaidi kutoka kwa Miss Tanzania 2000, Jacqueline Ntuyabaliwe.
Meya wa Ilala, Mh.Jerry Silaa (kuli), akimkabidhi tuzo ya Mtangazaji wa Runinga wa Kike Anayependwa Zaidi, Salama Jabir.
Elizabeth Michael ‘Lulu’, akitoa neno la shukurani baada ya kutwaa Tuzo ya Muingizaji Bora wa Kike Anayependwa Zaidi.
Mbunifu wa mavazi nchini,
Mustafa Hassanali (kulia), akikabidhi tuzo ya Mwimbaji wa Kike
Anayependwa Zaidi iliyonyakuliwa na Lady Jay Dee ambapo ilichukuliwa na
mwakilishi wake, Pot Fedha.
Salim Kikeke (kushoto), akipokea tuzo ya Mtangazaji wa Runinga Anayependwa Zaidi.
Waandaaji wa tuzo hizo, Nancy
Sumari (kushoto) na mumewe, Lucas Neghest wakitoa neno la shukrani muda
mfupi kabla ya shughuli za utoaji tuzo kuanza.
Mdogo wa marehemu Steven
Kanumba, Seth Bosco wa kwanza kushoto na Jacqueline Wolper wakipokea
tuzo ya Filamu Inayopendwa Zaidi ya Ndoa Yangu aliyocheza marehemu
pamoja na Wolper.
Meneja wa Kundi la Tip Top
Connection, Babu Tale (kushoto), akipokea tuzo ya Mwimbaji Bora wa Kiume
kwa niaba ya Diamond ambaye yupo safarini. Anayemkabidhi ni mtangazaji,
Salama Jabir.
Mratibu wa Shindano la Bongo Star Search, Rita Poulsen (kulia), akimkabidhi tuzo ya Muongozaji Bora wa Video za muziki, Nisher.
Msanii wa filamu nchini, Jacob Steven ‘JB’, (kushoto), akiteta jambo na mchekeshaji King Majuto.
MASTAA mbalilmbali kutoka kwenye tasnia tofautitofauti hapa nchini,
akiwemo Amri Athumani 'King Majuto', Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Millard
Ayo, usiku wa kuamkia leo wameng’ara vilivyo kwenye sherehe za utoaji
wa Tuzo za Watu ambazo zimefanyika kwa mara ya kwanza ndani ya Ukumbi wa
Serena, Posta jijini Dar es Salaam.
King Majuto ameibuka kidedea baada ya kutwaa Tuzo ya Muigizaji wa
Kiume Anayependwa Zaidi, huku Lulu akitwaa tuzo ya Muigizaji wa Kike
Anayependwa Zaidi, Millard Ayo alikamata tuzo mbili; Mtangazaji wa Redio
Anayependwa Zaidi na Kipindi cha Redio Kinachopendwa Zaidi.
Wengine walioibuka na tuzo hizo ni Nasibu Abdul ‘Diamond’, ambaye
ametwaa tuzo ya Video Bora ya Muziki Inayopendwa Zaidi huku Judith
Wambura 'Lady Jaydee akitwaa tuzo ya Msanii wa Muziki wa Kike
Anayependwa Zaidi, Salimu Kikeke akaondoka na tuzo ya Mtangazaji wa
Runinga wa Kiume Anayependwa Zaidi na Salama Jabir akachukua tuzo ya
Kipindi cha Runinga Kinachopendwa Zaidi.
Aidha, Prodyuza Nisher alitwaa tuzo ya Muongozaji wa Muziki
Anayependwa Zaidi na tuzo nyingine ilikuwa ya Filamu Inayopendwa Zaidi,
Ndoa Yangu.
No comments:
Post a Comment