Baba wa marehemu (kushoto) akilia kwa uchungu.
Timbwili! Katika hali ya kusikitisha mgonjwa Yasin
Jailan (15) aliyekuwa wodini anadaiwa kukata roho huku dokta akizichapa
kavukavu na wagonjwa, Ijumaa Wikienda limenasa kisa cha ajabu.
Mwili wa marehemu Yasin Jailan
(15) aliyekata roho ndani ya wodi namba tisa katika Hospitali ya Rufaa
ya Morogoro huku dokta akizichapa kavukavu.
Akiwa mitaani akisaka matukio, mwanahabari wetu alivutiwa waya na chanzo
chetu kisha akatonywa kuwa kuna bonge la timbwili kwenye wodi namba
tisa katika Hospitali ya Rufaa ya Morogoro ambapo alitii wito na kufika
eneo la tukio ndani ya dakika sifuri (huwa Global hatulazi damu kufika
eneo la tukio).
Alipofika wodini hapo, mwandishi wetu alishuhudia
mtoto akikata roho huku baba mwenye mgonjwa aliyetajwa kwa jina la
Jailan Mrisho akizichapa na daktari ambaye jina halikupatikana.
Dada wa marehemu naye akiwa hospitalini hapo.
Kwa mujibu wa baba mwenye mgonjwa, alimfikisha mwanaye hospitalini
hapo akisumbuliwa na ugonjwa wa malaria uliokuwa umepanda kichwani na
kusababisha kuanguka ovyo.
Alidai kuwa baada ya vipimo vya mwanaye walishauriwa kwenda kununua dawa ambazo ziliwagharimu shilingi elfu arobaini.
Alisema walipofanikiwa kupata fedha na kununua dawa hizo, daktari
alidaiwa kumuuzia mgonjwa mwingine hivyo kusababisha timbwili hilo.
Baadhi wanachi waliojaa hospitalini kushuhudia mkasa huo.
Baada ya kuona hali tete huku watu wakiwa na hasira wakimlalamikia
daktari huyo kwa uzembe, mwanahabari wetu alipiga simu kituo kikuu cha
polisi mkoani hapa ambapo polisi wa pikipiki almaarufu kama tigo
walifika na kumchukua daktari huyo kisha kumkimbiza kituoni kumnusuru na
kipiga kutoka kwa watu wengine ambao walifika hospitalini hapo kuwaona
wagonjwa wao.
Kaimu kamanda wa polisi mkoani hapa, John Laswai alithibitisha
kutokea kwa tukio hilo na kwamba jeshi la polisi linaendelea na
uchunguzi baada ya kumnusuru dokta huyo ambaye kwa sasa anadunda mtaani.
Daktari akikimbizwa kituo cha polisi ili kuepushwa na kipigo kutoka kwa wananchi wenye hasira kali.
Hadi gazeti hili linakwenda mitamboni, mipango ya mazishi ya marehemu
ilikuwa ikifanyika nyumbani kwao maeneo ya Mkuyuni mkoani hapa.
Uchunguzi wa Ijumaa Wikienda umebaini kwamba kumekuwa na vifo vingi
vinavyosababishwa na madaktari ambao hawana wito wa kazi hiyo hivyo
serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii chini ya waziri wake,
Dk. Seif Selema Rashid kuchukua hatua juu ya suala hilo.
No comments:
Post a Comment