Staa wa Bongo fleva, Diamond Platinumz akipozi na mpenzi wake Wema Sepetu ndani ya Ukumbi wa ICC, Durban nchini Afrika Kusini.
WAMUACHE! Hii ndiyo kauli pekee ambayo unaweza kuisema
kwa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kwani Jumamosi iliyopita
alifanya maajabu na kuishangaza dunia kufuatia shoo kali aliyoangusha
katika Tuzo za MTV Africa (Mama) 2014 katika Ukumbi wa ICC, Durban
nchini Afrika Kusini.
Diamond, Wema, Babu Tale na Aunt Ezekiel katika pozi.
Diamond aliyeambata na timu ya wasanii tofauti kutoka Bongo wakiwemo
waigizaji na mameneja wake, licha ya kukosa tuzo alizokuwa akiwania
yaani kipengele cha Mwanamuziki Bora wa Kiume na Wimbo Bora wa
Kushirikiana, alikuwa gumzo kwa kupiga shoo kali akishirikiana na David
Adeleke ‘Davido’ wa Nigeria.
...Diamond na Wema.
Awali, shoo hiyo ilianza saa nne usiku ambapo Diamond aliyeambatana
na ubavu wake, Beautiful Onyinye, Wema Sepetu walikuwa kivutio katika
‘red carpet’ ambapo walipoingia wakiwa wamekumbatiana, watu walipiga
kelele kuashiria kuwa wanaikubali kapo hiyo.
Miongoni mwa shoo za
awali ambazo ziliamsha hisia za mashabiki waliofurika ukumbini humo ni
ya Kundi la Mafikizolo ambayo lilishangiliwa sana.
Wa kwanza kunyakua tuzo ya Mwanamuziki Bora Chipukizi ni Stanley Enow
wa Nigeria. Tuzo ya Mwanamuziki Bora wa Kike ilienda kwa Tiwa-Savage wa
Nigeria na Mwanamuziki Bora wa Hip Hop ilienda kwa Sarkodie wa Ghana.
Muonekano wa Jumla, tuzo ilitua kwa mwanadada Lupita Nyong’o wa Kenya.
Kwenye kipengele cha Kundi Bora la Mwaka, tuzo ilikamatwa na
Mafikizolo ambao waliwatupa kapuni P- Square, Sauti Sol, Mi Casa na Big
Nuz.
Davido aliibuka Mwanamuziki Bora wa Kiume wa Mwaka na kuwagalagaza
akina Diamond, Wizkid, Anselmo Ralph na Donald. Kipengele cha Wimbo Bora
wa Kushirikiana, tuzo ilitua kwa Uhuru aliyeshirikiana na DJ Buckz,
Oskido, Professor na Yuri da Cunha.
Hapo ndipo alipopanda mkali kutoka Marekani, Trey Songz ambaye
alipewa shangwe za kutosha hususan alipopiga wimbo wake wa Nana kisha
jukwaa likakamatiwa na Diamond na Davido ambao walipafomu wimbo wa
Number One Remix ambapo mtoto huyo wa Tandale alipagawisha mashabiki
wote kwa kuonesha staili tofauti za kucheza kabla ya kumuacha stejini
Davido aendeleze makamuzi.
Diamond na Davido waliingia kwa staili ya aina yake ya kuzuiwa na
warembo mlangoni, wakavamia jukwaa kwa spidi na kufanya umati uwe bize
kwa dakika kadhaa wakati shoo hiyo ya nguvu ikiendelea.
No comments:
Post a Comment