MAKUBWA! RB nambari TBT/RB/3478/2014 ya Kituo cha
Polisi Tabata, jijini Dar es Salaam ina kesi ya dereva taksi
aliyepatikana kwa jina moja la Lindoya akidaiwa kuharibu mali za Asia
Hakika kwa sababu eti alinyimwa unyumba, Uwazi linakuhabarisha.
Asia Hakika anayedai kuharibiwa mali zake na dereva taksi aitwaye Lindoya.
Mlalamikaji Asia, mkazi wa Tabata – Chama na mtuhumiwa Lindoya mwenye
makazi yake Mbezi – Makabe ni wapenzi wa muda mrefu sasa, lakini baada
ya Asia kugundua kuwa mwenzake ana mke na watoto, akagoma kumpa tendo la
ndoa, jambo lililoibua kisanga hicho.
Akizungumza na Uwazi, Asia alisema: “Lindoya ni mpenzi wangu,
tulikuwa tunaelekea kuwa mume na mke, maana tumeishi kwa miaka miwili
sasa, lakini siku zote amenieleza kuwa hana mke wala watoto, lakini
nimegundua kuwa alinidanganya.
Asia Hakika akiangalia mali zake zilizoharibiwa.
“Ana mke na watoto wawili, nikaamua nimuache aendelee na familia
yake. Akakataa, anataka kunitumia tu. Nilipomkatalia ndiyo akaamua
kuniharibia vitu vyangu. Alinikuta nina vitu vya ndani nilivyonunua kwa
fedha zangu, nimepanga chumba kwa pesa yangu na aliniomba tuishi
pamoja nikamkubalia.
“Baadaye akaanza kujenga nyumba huko Mbezi ya Makabe, nilifurahi sana
niliamini kuwa tukioana tutakua tunaishi huko lakini cha kushangaza
baada ya kumaliza kujenga alimfuata mkewe huko Mbeya, wakahamia na
watoto wake.”
Alisema, mpenzi wake huyo zilipendwa, alimwambia asikanyage nyumbani
kwake kwa kuwa mkewe amekuja, jambo ambalo alikubaliana nalo kwa sharti
kuwa wasitishe uhusiano wao lakini Lindoya akaonekana kutoridhika.
Baadhi ya mali za Asia Hakika zilizoharibiwa.
“Siku moja nikiwa kazini, alifika nyumbani kwangu akafungua mlango
kwa funguo wake, maana kila mmoja alikuwa na wake; akaharibu mali zote
ndani, akaacha kitanda tu. Nimeumia sana kwa kweli,” alisema Asia.
Kwa sasa kesi hiyo ipo katika Kituo cha Polisi Tabata kwa uchunguzi
ambapo jalada la uchunguzi limeandikishwa kwa namba TBT/IR/2032/2014.
No comments:
Post a Comment