Rais Jakaya Kikwete alianza kwa kusema: “Watanzania hawapaswi kumbeza
Diamond kwani pamoja na kukosa tuzo ya MTV lakini kuna juhudi kubwa
alionyesha kwa kufanya shoo kubwa ya kwanza na ya kimataifa ambayo
niliishuhudia mwenyewe na niliona watu walifurahia sana,”
Rais Jakaya Kikwete akimpa
mkono wa pongezi Msanii mkali katika miondoko ya Bongo Fleva, Abdul
Nassib, Diamond kwa hatua aliyofikia.
“Diamond alilitangaza taifa letu kupitia shoo hiyo na muziki wetu wa
Tanzania, hivyo hatupaswi kuwa mbali na wasanii wetu kwani natambua wazi
Diamond bado yuko kwenye kinyang’anyiro cha tuzo za BET ambazo ni tuzo
kubwa sana nchini Marekani na naweza kusema kuwa hata kutambuliwa kwake
kuwepo kwenye tuzo hizo nalo ni jambo la kujivunia kwani uwepo wake ni
njia moja ya kulitangaza Taifa letu hata kama hatabahatika tena kuchukua
tuzo hizo,”
Diamond (kushoto) akiwa na mkali mwingine wa muziki kutoka Nigeria, maarufu kwa jina la Davido (aliye mbele pichani).
“Najaribu kuwatia sana moyo na kumwambia Diamond kuwa awe na
uvumilivu kwani nimeshaanza kuonyesha njia ya kumsaidia maana juzijuzi
nilimkuta Marekani na nilimkutanisha na mdau mkubwa sana wa muziki
duniani ambaye ndiye alimtoa Jay z, Usher Raymond na wasanii wengine
wakubwa na nilimuomba amsaidie kumwelekeza namna anavyoweza kukua kwenye
ulimwengu wa muziki”,
“Nimeshaongea na mmiliki wa kituo cha televisheni ya E ambayo ni
kubwa sana Duniani ikiwa ni njia mojawapo ya kuhakikisha naukwamua
muziki wetu, hivyo wanatarajia kuja Tanzania hivi karibuni akiwa
ameambatana na Usher Raymond na wadau wengine ambao watakuja kukutana na
kina Diamond na wasanii wa filamu ili wawape mbinu za kukuza sanaa
yetu,” alisema Rais Kikwete.
Diamond akiwa na Mpenzi wake Wema Sepetu.
Diamond alianza kubezwa na baadhi ya mashabiki na wasanii wenzake siku
chache baada ya kukosa tuzo na wengine walifanya hivyo siku ya uzinduzi
wa Wimbo wa Tulinde Utanzania ambapo walimtania kwamba hana uwezo wa
kuchukua tuzo hizo hivyo hata kwenye tuzo za BET asihangaike kwani
hatapata chochote.
No comments:
Post a Comment