Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. George
Simbachawene akiwa na wajumbe wa Bodi ya NHC na Watendaji wa NHC
walipotembelea mji wa Bunggol wenye nyumba za wananchi (social housing
estates) nchini Singapore kama sehemu ya ziara ya mafunzo.
Ujumbe wa Tanzania ukielezwa
namna mji wa Singapore ulivyopangwa kulingana na matumizi mbalimbali
ulipotembelea Mamlaka ya Uendelezaji Miji ya Singapore(URA) jana.
Ujumbe wa Naibu Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ukiwa katika Bodi ya Uendelezaji wa
nyumba ya Singapore ambayo harakati za Bodi hiyo zimewezesha asilimia
86 ya watu wa nchi hiyo kupata nyumba za kuishi. Nchi ya Singapore ina
watu milioni 5.4
Ujumbe wa Naibu Waziri ukiwa
katika kampuni inayosambaza na kusimamia usalama wa maji katika nchi ya
Singapore na maeneo mbalimbali Tanzania ya Hyflux Innovation Centre
ambayo pia imeonyesha nia ya kushirikiana na Tanzania kusambaza maji
katika maeneo inayojenga nyumba za wananchi.
No comments:
Post a Comment