Mrembo aliyekuwa akijihusisha na biashara haramu ya ngono nje ya ofisi za serikali akikurupuka mara baada ya kunaswa mtegoni.
Njaa mbaya! Kama ulikuwa unadhani ile Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya
Global Publishers imenywea, basi umenoa! Safari hii imenasa tukio la
mrembo akijihusisha na biashara haramu ya ngono nje ya ofisi za
serikali, Ijumaa Wikienda lina kitu laivu.
Tukio hilo lisilo la kimaadili lilijiri usiku wa manane wikiendi iliyopita kwenye ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Kijitonyama, Dar.
Baada ya kupokea kero kwa wakazi wazalendo wa eneo hilo kuwa ofisi
yao inanajisiwa, OFM ilifanya uchunguzi wake wa kina na ilipojiridhisha
ndipo ikaweka mtego.
Kabla ya tukio ilisemekana kuwa pamoja na ngono
kufanyika waziwazi na machangudoa waliopo maeneo mbalimbali ya Sinza na
Kijitonyama, Dar, siku hizi wadada hao wafikia hatua mbaya zaidi kwa
kufanyia maeneo yenye hadhi na sifa maalum kama viwanja vya shule za
msingi, nje ya ofisi za watu, karibu na misikiti na makanisani.
Timu ya OFM kazini ikimdhibiti mrembo huyo aliyekuwa akifanya biashara haramu.
“Yaani siku hizi hawa wasichana hawani soni hata tone, wamefikia
hatua ya kufanyia ngono sehemu rasmi tena bila kificho, kwa mfano pale
maeneo ya Sinza-Mapambano si wanafanyia ngono kwenye uzio wa shule!
Ukifika pale asubuhi utakuta kondomu kibao. Hata pale kwenye ofisi za
mtendaji utawaona wanafanyia ngono kule nyuma kwenye miti bila hata ya
hofu,” alisema mmoja wa wakazi wa Kijitonyama.
Tukirudi kwenye
tukio, OFM ikiwa doria chimbo, mishale ya saa nane na nusu usiku,
hakukuwa na purukushani yoyote iliyoonesha viashirio vya ngono nje ya
ofisi hiyo
Mrembo huyo akiwa chini ya ulinzi wa kachero mara baada ya kunaswa.
Ghafla nusu saa baadaye makamanda wa OFM waliokuwa katika kufunga
vifaa vyao vya kazi, walishuhudia Bajaj ikisimama mbele na kumshusha
mrembo mmoja maarufu kwa jina la Shishi akiwa na ‘mteja’ kisha
wakajibanza kwenye miti nje ya ofisi hiyo.
Makamanda wa OFM walikuwa makini kufuatilia mchezo mzima ambapo
waliwashuhudia wawili hao wakitandika khanga tayari kwa ajili ya ‘mambo
yao’.
Baada ya kila kitu kuwa sawa ndipo makamanda walipiga simu kwa
askari wa doria waliokuwa maeneo hayo na kuwavamia kisha kuwatia
nguvuni ambapo katika kujitetea mrembo huyo alisema kuwa, mteja wake
alimlazimisha kufanyia ngono katika eneo hilo kwa sababu alimaliza fedha
zote kwa kumnunua yeye pombe.
Askari akimuingiza mrembo huyo kwenye gari kumpeleka kituoni.
“Najua eneo hili ni la serikali lakini huyu jamaa alikuwa na fedha
kidogo na nyingine ya gesti nikaamua bora yote anipe mimi kisha
nikamleta hapa. Nisameheni sitarudia,” alisema mrembo huyo huku mteja
wake aliyeonekana kukolea kinywaji akiomba aachiwe kwa kuwa hakujua
alilokuwa akilifanya.
Hadi OFM inaondoka eneo la tukio wawili hao
walikuwa wametaitiwa mikononi mwa polisi ambapo kwa kawaida kisheria
watashitaki kwa kosa la uzembe na uzururaji.
Alipotafutwa Mtendaji wa Kata ya Kijitonyama ili kuzungumzia ishu
hiyo hakupatikana hewani na hata alipofuatwa ofisini kwake kulikuwa na
kufuli kubwa.
GPL
No comments:
Post a Comment