Oohoo nooo! Wakati aliyekuwa mumewe, George Otieno Okumu ‘Tyson’ (41) akipumzishwa kwenye nyumba ya milele huko Kisumu nchini Kenya, Yvone-Cherry Ngatikwa ‘Monalisa’ amewacharukia watu waliodai alikuwa akijipendekeza msibani ili kupata mirathi ya mwanaume huyo.
Awali, Mona ambaye ni staa mkubwa wa sinema za Kibongo alianza kutupia mitandaoni picha za kumbukumbu (mastaa wanaita Throw Back Thursday au TBT) akiwa na Tyson kuanzia siku ya send-off yake Agosti 14, 2001 na ile ya siku ya harusi yao Agosti 25, 2001.
Picha hizo ziliambata na maneno ikionesha ni kwa jinsi gani Tyson au baba Sonia (mtoto wao) alivyokuwa mtu muhimu maishani mwake.
Ishu hiyo ndiyo iliyosababisha tafrani kubwa huku akiambulia kushambuliwa kwa maneno makali kuwa anajipendekeza.
Muigizaji wa Bongo Muvi, Yvone-Cherry Ngatikwa ‘Monalisa’ akiwa na mwanaye, Sonia.
Habari za kiintelijensia zilidai kuwa kati ya wanawake wanne aliowaacha Tyson, pamoja na kutengana mwaka 2006 bila talaka, Mona ndiye amekuwa akipewa pole badala ya wanawake hao wengine akiwemo Beatrice, Angel na Lucy.
Kuna madai mazito yanayorushwa kwamba ishu ya mirathi ya Tyson inazidi kuzua tafrani kila mmoja akijiaminisha kuwa ndiye mrithi halali.Baada ya kuona maneno yanakuwa mengi ndipo Mona akacharuka na kuandika kwa kile anachokijua juu ya ishu hiyo.
Aliandika: “Let me clear the air. Ni hivi, pamoja na ujinga tulioufanya mimi na George katika maisha yetu, kwa macho ya kibinadamu utasema alikuwa na mke mwingine lakini kwa macho ya ki-Mungu, mimi ni mke halali wa George Otieno Okumu aliyelala.
Monalisa akiwa na aliyekuwa mume wake, George Otieno Tyson wakati akiwa hai.
Anayesema mke wa Tyson alijifungia ndani mimi nikawa nachukua pole zisizo zangu, dah! Kwanza wanawake walikuwa wawili ndani siyo mmoja na wote walijifungia ndani. Kwa nini? Ni Wakristo na wanaijua dini. Waombolezaji walikuwa wakinipa pole mimi. Ni kwa nini?
Jiulize kabla ya kuropoka halafu wewe ni mwanamke kuna siku yatakukuta.
Nilienda (msibani) kutimiza wajibu wangu kama mke, ningelia peke yangu kwetu mngenisema sana, nimekaa msibani naambiwa nachukua pole za bure.
Acha nikukumbushe maandiko... Alichokiunganisha Mungu?....(binadamu asikitenganishe). Kilichofungwa duniani?.....(kimefungwa na mbinguni) Nikupende, nikutunze hadi kifo?.....(kitakapotutenganisha).
Sasa kifo kimetutenganisha. Siku ya mwisho unadhani George ataitwa na nani? Pamoja na mambo yake yote acheni nimlilie, he was a good father kwa Sonia wangu especial miaka 5 ya mwisho wa uhai wake.
Acheni nimlilie, he was my best friend 1998-2014. Nime-share naye kitanda 2000-2006. Nitakuwa mtu wa aina gani nisiwe na uchungu?
Ukiona mwanamke mwenzio kaishindwa ndoa, usimcheke jua kuna sababu...na ni fundisho kwa wachukua waume za watu wote mjini.
Mume akiumwa huwa anarudi kwa mkewe na akifa? And for your info...msianze anajifanya mke sasa hivi ili apewe mali...
Sonia ni mali kubwa sana aliyoniachia, am so happy. Waache wao wanaolilia kupewa pole wapiganie. Mwenyewe aliyetafuta kafa kaziacha, sembuse tuliobaki?
“Niacheni nimlilie, waacheni fans wangu walie na mimi.”
Hata hivyo, baadhi ya mashabiki wake walimshauri kuwa angenyamaza na kuacha watu wazungumze kwani ni upepo tu unapita hivyo naye aliwasikiliza na kuamua kuondoa maneno hayo katika kurasa zake kwenye mitandao ya kijamii.
Tyson ambaye alikuwa bonge la mwongozaji wa vipindi vya runungani na sinema za Kibongo alifariki dunia kufuatia ajali mbaya ya gari aina ya Toyota Noah, iliyotokea eneo la Gairo mkoani Morogoro ambapo Jumamosi iliyopita alizikwa kijijini kwao huko Kisumu nchini Kenya.
No comments:
Post a Comment