Flora Mbasha akiwa na mumewe Emmanuel Mbasha.
MSANII Emmanuel Mbasha (32) na mume wa
Mwimbaji wa Injili, Flora Mbasha jana amepandishwa katika Mahakama ya
Wilaya ya Ilala akikabiliwa na mashitaka mawili ikiwemo ya ubakaji.
Mshtakiwa huyo ambaye ni mfanyabiashara na mwimbaji alisomewa
mashitaka yake mbele ya Hakimu Mkazi Wilberforce Luago. Wakili wa
Serikali Nassoro Katuga alidai kuwa mshtakiwa alitenda makosa hayo
mawili maeneo ya Tabata Kimanga, jijini Dar es Salaam.
Katuga alidai katika shitaka la kwanza kuwa, Mei 23, mwaka huu eneo la
Tabata Kimanga, Wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam, kinyume cha
sheria huku akijua ni kosa alimuingilia kwa nguvu msichana anayedaiwa
kuwa shemeji yake (jina limehifadhiwa).
Katika shtaka la
pili, ilidaiwa kuwa Mei 25, mwaka huu eneo la Tabata Kimanga, jijini
Dar es Salaam, kinyume cha sheria, mshtakiwa aliumuingilia kwa nguvu
mfanyakazi wake (jina limehifadhiwa). Hata hivyo, mshtakiwa alikana
mashitaka hayo .
Upande wa Jamhuri ulidai kuwa hauna
pingamizi la dhamana. Hakimu Luago alitaja masharti ya dhamana kwa
mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili, mmoja awe mtumishi wa serikali na
mwingine kutoka taasisi inayotambulika watakaosaini hati ya dhamana ya
Sh. milioni 5.
Mshtakiwa alishindwa kutimiza masharti ya
dhamana hivyo alipelekwa rumande na kesi iliahirishwa hadi Juni 19,
mwaka huu itakapotajwa. Mbasha akiwa chini ya ulinzi wa askari polisi
alisindikizwa katika basi la Jeshi la Magereza kwa ajili ya kwenda
kuanza maisha mapya mahabusu ya Keko, jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment