Basi lililombeba Emmanuel Mbasha likiwa chini ya ulinzi mkali wa askari magereza likisindikizwa kuelekea mahakamani.
HAKUNA neno jingine zaidi ya kusema maskini Mbasha!
Jina zima ni Emmanuel Mbasha (32) ambaye ni mume wa mwimba Injili
Bongo, Flora Mbasha juzi amepandishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala
jijini Dar es Salaam ishu ni yale madai ya kumbaka mara mbili shemeji
yake (jina lipo).
Akisomewa mashitaka mbele ya hakimu mkazi wa mahakama hiyo,
Wilberforce Luago, Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga alidai mshitakiwa
huyo alitenda makosa hayo mawili maeneo ya Tabata- Kimanga jijini Dar es
Salaam.
Katika shitaka la kwanza, Wakili Katuga alisema Mei 23, mwaka huu,
huko Tabata- Kimanga jijini Dar, mtuhumiwa huku akijua ni kinyume cha
sheria alimwingilia kwa nguvu msichana anayedaiwa kuwa ni shemeji yake.
Katika shitaka la pili, wakili huyo alisema Mei 25, mwaka huu
hukohuko Tabata Kimanga, mshitakiwa alimwingilia tena kwa nguvu shemeji
yake huyo huku akiendelea kujua ni kinyume cha sheria.
MBASHA AULIZWA, ATOA NENO
Hata hivyo, mshitakiwa huyo alipotakiwa kusema kweli si kweli mahakamani hapo, alisema si kweli.
SERIKALI YASEMA HAINA PINGAMIZI YA KUWA HURU
Baada ya kutamka neno hilo, upande wa Jamhuri ulitoa hoja kwamba hauna
pingamizi la dhamana kwa mshitakiwa hivyo, Hakimu Luago alitaja masharti
ya dhamana kwa mshitakiwa.
Hakimu huyo alisema ili mshitakiwa awe huru kwa dhamana alitakiwa
kuwa na wadhamini wawili. Mmoja kati ya wadhamini hao awe mfanyakazi wa
serikalini, mwingine atoke kwenye taasisi inayotambulika. Wote kama
wapo, walitakiwa kusaini hati ya dhamana ya shilingi milioni 5 kwa kila
mmoja.
MBASHA AENDA KEKO
Hata hivyo, mshitakiwa huyo
alishindwa kutimiza masharti ya dhamana hiyo hivyo hakimu aliamuru
apelekwe kwenye Mahabusu ya Keko jijini Dar ambako atakuwa chini ya
ulinzi. Mbasha aliondolewa mahakamani hapo akiwa chini ya ulinzi mkali
wa polisi.
Kwa mujibu wa habari kutoka mahabusu, juzi baada ya
kufikishwa magereza, mtuhumiwa huyo alikesha akilia na kusali ili janga
hilo limwepuke, lakini si kama atakavyo yeye bali mapenzi ya Mungu
yatimizwe.
LEO ANARUDI TENA
Ni kama shughuli imeanza kwani,
hakimu alisema leo (Juni 19) mshitakiwa alitakiwa kurudi tena
mahakamani hapo ambapo kesi yake itatajwa tena.
FLORA ANAPOKEAJE TAARIFA ZA MUMEWE?
Mwandishi
wetu alimsaka Flora ili azungumzie madai ya mumewe kupandishwa
mahakamani ambapo alisema hana mawasiliano kabisa na Mbasha kwa hiyo
hajui chochote kuhusu habari hizo.
AMANI: “Sasa ndiyo unaambiwa, wewe unazipokeaje taarifa hizo?”
FLORA: “Hizo habari sizijui kama nilivyosema.”
Jumatatu iliyopita, mwandishi wetu aliipiga namba ya Mbasha, simu
ilipokelewa na mtu mwingine ambaye alipoulizwa alipo Mbasha, alijibu
hayupo kisha akakata simu.
Baada ya hapo, kila mwandishi wetu alipopiga simu hiyo haikupokelewa mpaka siku ilipoisha.
Jumanne iliyopita kabla Mbasha hajapanda kizimbani, mwandishi wetu
alipiga tena simu hiyo ikapokelewa na mtu yuleyule wa jana yake lakini
safari hii akawa mvumilivu, kwani hakukata simu haraka. Mazungumzo
yalikuwa hivi;
MWANDISHI: “Kaka habari yako?”
MPOKEA SIMU: “Njema, nani mwenzangu?”
MWANDISHI: “Mimi ni … (mwandishi alijitambulisha kwa jina lake), naweza kuzungumza na Mbasha?”
MPOKEA SIMU: “Mbasha huwezi kuzungumza naye kwa sasa, ametoka.”
MWANDISHI: “Saa ngapi atakuwa amerudi?”
MPOKEA SIMU: “Mwenyewe akiwa tayari atakupigia, nitamwambia.”
MWANDISHI: “Oke, sawa.”
NI KASHFA YA AINA YAKE
Sakata la Mbasha,
liliibuliwa na kashfa kwamba mume huyo alimbaka mara mbili shemeji yake
huyo ambaye alitoa taarifa kwenye Kituo cha Polisi Tabata Shule jijini
Dar.
Hata hivyo, polisi walipokwenda kumkamata nyumbani kwake
hawakumkuta na baada ya hapo alitoweka jumla mpaka Jumatatu iliyopita
ambapo inadaiwa alikuwa akiishi kwa mdogo wake, Mbezi, Dar.
Kashfa hiyo ndiyo iliyoibua tuhuma kutoka kwa Mbasha akisema kuwa
Mchungaji Gwajima alimuhifadhi mkewe nyumbani kwake baada ya yeye
kukumbwa na tuhuma hiyo ya kubaka madai ambayo mtumishi huyo wa Mungu
aliyapangua vizuri na Flora akabainika kwamba anaishi hotelini, Sinza
jijini Dar.
GPL
No comments:
Post a Comment