Friday, June 27, 2014

MTITU AKIRI BOTI KUMTOA USHAMBA

BIG Boss wa Kampuni ya Five Effect, William Mtitu amesema amekoma kutumia usafiri wa boti kwani ulimfanya akose amani juzikati walipokwenda Zanzibar katika Tamasha la Ziff.

 Boss wa Kampuni ya Five Effect, William Mtitu
 
Akipiga stori mbili tatu na paparazi wetu, Mtitu alisema alipokuwa safarini, boti ilimtoa ushamba baada ya hali ya hewa kumshinda na kutapika sana akiwa humo.
“Boti imenitoaje ushamba yaani nimetapika njia nzima tangu naanza safari hususan kutoka Zanzibar hadi nilipokaribia kufika Dar ndio nikaacha kutapika huku nikiwa nimeshikiliwa na Rich na Barafu, sipandi tena aisee,” alisema Mtitu.

No comments:

Post a Comment