Tuesday, June 10, 2014

MHUSIKA WA PICHA CHAFU ZA MHESHIMIWA KOMBA AIBUKA NA KUFUNGUKA YA MOYONI

Angel Kissanga, mkazi wa Kinondoni jijini Dar anayedaiwa kupiga picha tata na mheshimiwa Komba.

SIKU chache zimekatika baada ya tukio la kusambaa mitandaoni kwa picha tata zenye pozi kati ya mheshimiwa Komba na mrembo aliyejulikana kwa jina moja la Angel.

Hatimaye mrembo huyo ameibuka na kuanika mambo mazito kama si makubwa, Risasi Mchanganyiko linakudadavulia.

Awali katika gazeti hili toleo la Jumamosi iliyopita ukurasa wa mbele kulikuwa na habari hiyo ikiwa na kichwa; KHAA! KOMBA! Katika habari hiyo picha zilizomuonesha mheshimiwa Komba akiwa na mrembo huyo zilipamba ukurasa huku mwenyewe (Komba) akidai ni picha za kutengeneza).
OFM YAINGIA MITAANI
Kwa vile Komba alikataa picha si zake huku baadhi ya vyombo vya dola kama Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) vikitangaza kuingia kazini kumtafuta sosi wa picha hizo, ilibidi timu makini ya Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ kutoka Global Publishers iingie kazini kumsaka mrembo huyo kwa udi na uvumba.


  Mheshimiwa Komba.

 YATUMIA NUSU SIKU
OFM ambayo huwa haishindwi kitu, ilitumia nusu siku ya Ijumaa iliyopita na kufanikiwa kuinasa namba ya simu ya mkononi ya Angel pamoja na picha nyingine ikiwepo iliyotumika ukurasa wa mbele wa gazeti hili.

Aidha, ilibainika kwamba, mrembo huyo anaitwa Angel Kissanga, mkazi wa Kinondoni jijini Dar es Salaam, bila ajizi Paparazi wetu alimwendea hewani Angel na kumuuliza kama ana habari zozote kumhusu yeye.
Angel: “Habari kama zipi? Mimi sina habari zozote.”

Paparazi: “Hujaona kwenye mitandao ya kijamaii wameweka picha zako ukiwa katika mapozi tata na mheshimiwa Komba?”
Angel: “Ngoja kwanza, nitakupigia.”

MUDA UNAKWENDA, ANGEL ARUDIWA
Baada ya kuona muda unakatika bila mrembo huyo kupiga simu kama alivyokuwa ameahidi, paparazi wetu alimrudia hewani ambapo safari hii simu yake ilipokelewa na mwanamke aliyejitambulisha kuwa ni dada wa Angel.


 Angel Kissanga katika pozi na mheshimiwa.

“Mimi si Angel, ni dada yake. Angel amepandwa na presha baada ya wewe kumwambia kuna picha zake na mheshimiwa Komba kwenye mitandao.
“Unajua ngoja nikuambie ukweli. Mdogo wangu ameshtuka sana, hivi hapa tupo Hospitali ya Micco Sinza, amelazwa.”

PAPARAZI ATIA TIMU HOSPITALINI
Kusikia hivyo, paparazi wetu alifunga safari hadi kwenye hospitali hiyo ambapo kweli mrembo huyo alikuwa amelazwa kwa matatizo ya presha ya kupanda.

Mwanamke aliyejitambulisha kuwa ni mama mdogo wa Angel alimjia juu paparazi wetu akidai yeye ndiyo chanzo cha mwanaye huyo kupandwa na presha ghafla, akamtimua asimuone mgonjwa.


 MAZUNGUMZO YA BAADAYE
Siku iliyofuata, paparazi alibahatika kuzungumza na Angel ambaye aliweka wazi mambo yake kuhusu picha hizo kama ifuatavyo:

“Mimi nataka kusema kwamba picha nimeziona, nazifahamu kweli ni mimi.”
Paparazi: “Ni kweli ulipigwa ukiwa na mheshimiwa Komba?”
Angel: “We jua tu kwamba picha nazijua. Zilipigwa na simu ya LG.”
Paparazi: “Alipiga nani?”

Angel: “Nimesema nazifahamu.”
Paparazi: “Hiyo simu ni ya nani?”
Angel: “We wa nini?”


 Angel Kissanga.

 Paparazi: “Okey, mheshimiwa Komba unamfahamu?”
Angel: “Namfahamu ndiyo.”
Paparazi: “Ni nani wako?”

Angel: “Nimekwambia namfahamu.”
Paparazi: “Sasa mbona mheshimiwa Komba anasema picha zimetengenezwa?”
Angel: “Mimi sijui sasa.”

ANGEL ATAKIWA KUTIA TIMU GLOBAL
Baada ya mazungumzo hayo, paparazi alimtaka msichana huyo kufika kwenye ofisi za magazeti ya Global ambapo alikubali.

Hata hivyo, baadaye alisema amebatilisha baada ya baba yake kuingilia kati sakata la picha hizo akidai yeye ndiye atakuwa msemaji mkuu.
Habari za chini kwa chini zilidai kwamba, kusita kuweka miguu kwa Angel kwenye ofisi za Global kulitokana na zuio la mheshimiwa mmoja ambaye alimchimba mkwara kwamba asitoe ushirikiano wowote na vyombo vya habari.

MASWALI MUHIMU
Maneno ya Angel na mheshimiwa Komba yanapingana. Mmoja anasema picha zilitengenezwa, mwingine anazitambua na zilipigwa kwa simu ya LG, nani mkweli? (endelea kufuatilia Magazeti Pendwa ya Global Publishers).

ANATAJWA PAULINA
Mbali na kupishana kwa maneno ya wawili hao, mwanamke mmoja aliyetajwa kwa jina moja la Paulina anatajwa kuwa nyuma ya sakata hilo.

Mwanamke huyo anadaiwa wakati fulani kuingia kwenye mzozo na Angel na akaja kudai ameipata simu yenye picha za mrembo huyo na mheshimiwa bila kujulikana alikoipata. Je, aliipata kwa Angel au mheshimiwa Komba? (endelea kusoma magazeti ya Global).
Ni mzozo gani aliokumbana nao Angel kwa Paulina? Unaweza kuwa wa wivu wa mapenzi? Na kama ni wivu wa mapenzi walikuwa wanamgombea nani? (Endelea kutembelea hapa).


 UTATA KUHUSU KOMBA
Katika mahojiano na Risasi, Komba alipopigiwa simu kwa mara ya kwanza, Alhamisi mchana wa saa 7 baada ya kutoka bungeni, kabla ya kuelezwa sababu za kupigiwa simu, alijibu anajua alichopigiwa simu. Alijuaje?

Aidha, Komba alisema anazijua zile picha lakini yule msichana hamtambui. Kivipi? (Endelea kufuatilia hapa).
Komba alisema anazo picha nyingine akiwa kwenye pozi la kawaida bila yule msichana, alipotakiwa kuzituma kwa mwandishi ili ajiridhishe, alikataa! Kwa nini? (Usikose kuendelea kutufuatilia).

Achana na maneno ya kwenye mitandao ya kijamii, Komba alipohojiwa na kituo kimoja cha redio, Ijumaa asubuhi, akasema anajua zile picha zimetengenezwa na wabaya wake, lakini akasema anamwachia Mungu. Kwa nini amwachie Mungu jambo zito kama hilo?
MAGAZETI YA GLOBAL
OFM ni kitengo rasmi, makini kilicho ndani ya Global. Hakijawahi kushindwa. Kimefichua uovu mwingi sana unaofanyika kwenye jamii. Kwa hili la Komba na Angel, ni dogo sana. Tunaahidi kuendelea kufuatilia na tutaanika ukweli halisi wa kila kinachoendelea.

Magazeti pendwa ya Global ni Amani, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Uwazi na Risasi. Hakikisha hukosi nakala yako. Tutakuwa wa kwanza kukuhabarisha ukweli halisi pengine kabla hata ya vyombo vya dola venye kila aina ya vifaa.

Source: GPL

No comments:

Post a Comment