Mwanamuziki Hafsa Kazinja anayetamba na Wimbo wa Mlala
Nje huku video yake ikiwa tayari, ameamua kuikacha dini yake ya Kiislam
na kuhamia kwenye Ukristo.Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Hafsa
alisema alifikia uamuzi huo baada ya kusumbuliwa na maruhani ambayo
yalimfanya arukwe na akili.
Mwanamuziki Hafsa Kazinja.
“Niliumwa sana hadi ikaonekana nimerukwa na akili, maruhani ndiyo
yaliyokuwa yananisumbua. Kuna kipindi yalikuwa yakiniambia nisile samaki
wala dagaa, mara yakaniambia natakiwa kuwa mganga.
“Njia zote ziligonga mwamba, nikaambiwa nisali na nimuachie Mungu,
nikawa nikisali sauti zinanijia nimtukane Mungu tena matusi makubwa,
nimeenda hadi kwa waganga, mashehe na walokole wakaniombea na nikapoteza
pesa nyingi hadi nikauza nyumba yangu na magari lakini wapi. Nimekwenda
Kanisa la Zoe ndiyo nimepona, namshukuru Mungu.
“Sasa nimeamua kuwa Mkristo, yaani nimebadili dini kwa kumaanisha,
nampenda Mungu katika roho na kweli. Sijabatizwa hivyo bado sijabadili
jina ila nasali Kanisa la Zoe lililopo Segerea jijini Dar.”
No comments:
Post a Comment