MAJANGA! Staa wa filamu na muziki Bongo, Isabela Mpanda
alijikuta akichezea kipigo kutoka kwa mke wa kigogo mmoja maarufu
jijini Dar baada kutuhumiwa kuwa anaiba penzi la bosi huyo.
Staa wa filamu na muziki Bongo, Isabela Mpanda akipozi.
Tukio hilo la aibu lilitokea mwaka 2010 ambapo chanzo cha staa huyo
kuumbuka kilikuwa ni meseji aliyomtumia kigogo huyo kisha mkewe kuinasa.
Mke huyo akaichukua namba ya Isabela na kuanza kumsaka na alipompata
akamuangushia timbwili.
Taarifa zinasema baada ya kuchezea kipigo hicho, Isabela alikiri
kutenda kosa hilo pasipo kujua yule jamaa alikuwa ni mume wa mtu.
Alipotafutwa Isabela, alisema anakumbuka tukio hilo ambalo lilimfanya tangu siku hiyo aogope kabisa waume wa watu.
“Daah! We acha tu tangu siku hiyo nilikuwa makini sana na waume wa watu maana nilipigwa pasipo kuwa na kosa,” alisema Isabela.
No comments:
Post a Comment