UBABE! Mwigizaji wa sinema za Kibongo, Wastara Juma
aliwahi kuzichapa kavukavu na dereva wa daladala baada ya kuoneshewa
ishara ya matusi.
Ishu ilikuwa hivi, miaka miwili iliyopita jijini Dar, Wastara alikuwa
na wasanii wenzake kituoni sasa daladala likapita karibu yao na
kummwagia maji na alipojaribu kumwambia kistaarabu kwamba hakufanya
‘fea’, dereva huyo akamuoneshea ishara ya matusi.
Mwigizaji wa sinema za Kibongo, Wastara Juma.
Wastara uvumilivu ukamshinda, akamvaa dereva huyo wa daladala na
kumkwida ndipo vurugu kubwa ilipotokea maana dereva huyo naye hakutaka
kukubali, alianza kujibu mashambulizi kabla wasanii waliokuwa na Wastara
hawajamuamulia.
Alipotafutwa Wastara na kuulizwa juu ya kisa hicho, alicheka sana na kudai alikumbushwa mbali:
“Hahahahahaha! Daah siku hiyo ilikuwa si mchezo alinimwagia maji tena
yenye matope halafu namwambia ananitukana palikuwa hapatoshi kama
tusingeamuliwa,
No comments:
Post a Comment