SKANDALI! Prizenta maarufu Bongo, Maimatha Jesse
amejikuta katika wakati mgumu baada ya kukwaa skendo ya utapeli kutokana
na dawa za kukuza maungo anazoziuza kuwa hazifanyi kazi.
Sosi ameibua utapeli huo wa Maimatha kwa kusema:
Prizenta maarufu Bongo, Maimatha Jesse akipozi katika duka lake la vipodozi.
“Maimatha anatapeli watu na dawa zake, yaani tumepaka mabinti wengi
hazitusaidii chochote, ni wizi mtupu, laki mbili bila chochote kweli
roho inauma.”
Maimatha Jesse.
Baada ya kunyaka madai hayo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Maimatha akakanusha:
“Hao wamejisikia tu kuongea hata siwafahamu na wala sijawahi kupata
kesi kama hizo, mbona nilishawauzia wengi? Mimi mwenyewe zimenisaidia,
wazushi tu,” alisema Maimatha.
No comments:
Post a Comment