Mwigizaji wa Bongo muvi, Vanitha Omary akitabasamu.
HAIJAKAA poa! Staa wa sinema za Kibongo, salome
Ndumbagwe Misayo ‘Thea’ na rafiki yake wa kitambo ambaye pia ni
mwigizaji, Vanitha Omary wamepishana kauli na kuchambana vilivyo msibani
kwa komediani mkongwe, Said Ngamba ‘Mzee Small’.
Ishu hiyo iliibuka mara baada ya Thea kumtuhumu Vanitha kumuita mume
wake mnafiki kwa kitendo cha kulikacha Shirikisho la Filamu Tanzania
(TAFF) na kujiunga na Bongo Movie Unity ndipo ‘kikanuka’.
Baada ya ugomvi kutulia, mwanahabari wetu aliwatafuta wawili hao, kila mmoja akaongea lake.
Vanitha: “Nimeumizwa na Thea, nahisi alikuwa na mambo mengine ndiyo
ameamua kunitungia...sidhani kama nitakuwa naye karibu tena.”
Mwigizaji wa filamu Bongo, salome Ndumbagwe Misayo ‘Thea’.
Thea: “Mimi sina muda wa kugombana na Vanitha kwani siyo saizi yangu nitagombana na mastaa wenzangu.”
No comments:
Post a Comment