Wednesday, June 18, 2014

HOFU YA BOMU YATANDA MLIMANI CITY.... WATEJA WATAHARUKI

 Walinzi wa maduka ya Mlimani City jijini Dar wakikagua kitu kinachosadikika kuwa ni bomu.

HUKU watu karibia 60 nchini kenya wakiuawa kwenye mashambulizi ya kigaidi, katika hali isiyo ya kawaida nchini Tanzania, walinzi wa Maduka ya Mlimani City jijini Dar wamejikuta wakipata mchecheto wa aina yake baada ya kitu kilichodhaniwa ni bomu kukutwa kwenye eneo la kuegeshea magari.

 ...Ukaguzi ukiendelea.

Taarifa za uwepo wa kifaa hicho ziliwafikia waandishi wetu waliokuwa wakipiga doria katika eneo hilo na haraka wakasogea karibu kuwashuhudia walinzi hao wa Kampuni ya Ulinzi ya Omega wakiwa wamekizunguka kifaa hicho kwa umakini mkubwa.
Walinzi hao walimuita kiongozi wao ambaye alifika na kukichunguza kifaa hicho ambapo alipokifungua aligundua ni betri bovu la pikipiki.Waliichukua betri hiyo na kuitupa huku wakitawanyika kurudi kwenye maeneo yao ya ulinzi.

 Eneo la Mlimani City.


No comments:

Post a Comment