Ohoo! Staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja amefunguka kuwa yuko
Bongo kwa kuwa ndipo nyumbani kwao lakini hana hamu ya kuendelea kuishi
nchini kutokana na kuzushiwa mambo kila kukicha.
Staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja
Akizungumza na Risasi Mchanganyiko wikiendi iliyopita, mwigizaji huyo alisema anapenda awe na maisha
ya furaha na wanawake wenziye kwa kubadilishana mawazo ya hapa na pale
lakini kwa sasa hana upendo huo kwa kuwa kuna watu wanaishi kwa
kutegemea bifu.
“Unajua inauma sana, unaenda klabu unamkuta mtu ambaye huko nyuma
alikuwa shoga’ko, kula, kuvaa na kila aina ya ushirikiano mnapeana, sasa
mnakuja kugombana, kiukweli roho huwa inauma ndiyo maana nashindwa hata
kwenda klabu kuepusha mengi, nasubiria viza yangu itoke nisepe zangu
China,” alisema Kajala.Kwa muda mrefu kumekuwa na ugomvi usiokwisha kati
ya Kajala na mwigizaji mwenzake, Wema Sepetu.
No comments:
Post a Comment