Gari aina ya Totyota Mark 2 iliyokuwa ikiendeshwa na kijana Deus baada ya kugonga ukuta wa nyumba karibu na barabara
Kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la Deus huko maeneo ya nane nane mkoani Morogoro asubuhi hii amesababisha uharibifu mkubwa wa mali baada ya kugonga nyumba ya Bi Tatu wakati akiwa naendesha gari la rafiki yake aliloazima kwa lengo la kwenda kuuza sura jirani na eneo anapoishi mpenzi wake. Wakati akiwa anarudisha gari ya watu ndipo aliposhindwa kukata kona kutokana na uwezo wake mdogo wa kuendesha gari na ndipo alipoigonga nyumba hiyo na kusababisha kubomoka upande mmoja.
Kijana Deus akiwa hajui la kufanya baada ya ajali hiyo
Baadhi wa mashuhuda wa ajali hiyo wakiwa wamelizunguka gari hilo katika eneo la tukio.
Wasamaria wema wakilisukuma gari hilo ili kulitoa katika eneo la ajali
Genge lililo katika nyumba iliyohusika na ajali hiyo
Baadhi ya majirani wakiwa katika eneo la tukio
Picha na habari zimetumwa na mwandishi wa Udaku Pepe Morogoro
No comments:
Post a Comment