KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, wadada wa mjini waliodaiwa kuwa machangu walimpa wakati mgumu, staa wa Bongo Dansi, Ally Choki ‘Mzee wa Farasi’ baada ya kumvamia jukwaani na kumfanyia mambo ya hovyo.
Staa wa Bongo Dansi, Ally Choki ‘Mzee wa Farasi’ akiimba pamoja na madada hao.
Tukio hilo lililoshobokewa na wanaume wakware, lilitokea wikiendi
iliyopita katika Ukumbi wa Meeda, Sinza – Mori, Dar ambapo mkali huyo
aliye Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo’ alikuwa
akiporomosha shoo ya nguvu na kundi lake.
Muziki ulipokolea wadada hao waliokuwa wamevalia nguo saresare
walikwenda jukwaani na kuanza kucheza kabla ya baadaye kuanza kujiachia
kihasarahasara.
Madada hao wakicheza kwa furaha.
“Mh! Hawa wadada vipi? Mbona wanaleta mambo ya Kanga Moko hapa? Cheza
gani ile ya aibu namna ile...hawa lazima ni machangu. Wamekosa wateja
sasa wamekuja kumtega Choki, maana mambo yale kama siyo machangu
utawaitaje?” alisikika dada mmoja akisema ukumbini humo.
Lakini hali ilikuwa tofauti kwa wanaume wakware ambao kwao ilikuwa
faraja kujionea mambo ya chumbani hadharani, kwani walikuwa
wakiwashangilia.
Hata hivyo, wakati wadada hao wakiendelea kufanya yao, Choki wa watu hakuwa na la kufanya, zaidi ya kuduwaa na kuwashangaa tu.
Madada hao wakilisakata rhumba pamoja na wapenzi wa bendi hiyo.
Ili kuonyesha kuwa vichwani mwao hamnazo, wadada hao hawakuona haya
kuachia maungo yao wazi, hata pale makufuli yalipobaki nje, walionekana
hawana habari kabisa.
Ilifikia mahali, mmoja wao akaenda mbali zaidi baada ya kutaka kuvua
nguo, hakupewa nafasi hiyo, mabaunsa walimbeba na kumtoa ili wastaarabu
waendelee kuburudika na Wazee wa Kizigo.
No comments:
Post a Comment