MAJANGA! Siku chache baada ya kuachiwa kwa dhamana
katika kesi ya kudaiwa kumbaka shemejiye, mwimbaji wa Injili na
mfanyabiashara Bongo, Emmanuel Mbasha amedaiwa kuibiwa hati za nyumba na
viwanja.
Mfanyabiashara Bongo, Emmanuel Mbasha mume wa Flora Mbasha.
Chanzo makini kilichomo ndani ya familia, kimedai kuwa mara baada ya
Mbasha kujitokeza na kuwekwa mahabusu Juni 17, mwaka huu, mtu
asiyejulikana alikwenda nyumbani kwa mfanyabiashara huyo,
Tabata-Kimanga, Dar na kukwapua hati za nyumba na viwanja mbalimbali
anavyovimiliki.
...Siku aliyopandishwa kizimbani.
“Mbasha hakukuta kitu pale nyumbani, vilikombwa vyote sijui na nani.
Inauma sana kwani mtu ndiyo kwanza ametoka mahabusu halafu anakuta
nyumbani kwake hakuna vitu muhimu kama hivyo, inasikitisha sana,”
kilisema chanzo hicho.
Kikizidi kumwaga data, chanzo hicho kilisema katika vitu vilivyoibwa
ni pamoja na nyaraka mbalimbali zikiwemo hati za viwanja kadhaa
vilivyopo Iringa, kadi ya gari na vitu vingine vidogovidogo.
Baada
ya kunyaka madai hayo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Mbasha ili kujua
ukweli wa ishu hiyo ambapo alipopatikana alikiri kutovikuta vitu hivyo
muhimu nyumbani kwake.
“Ni kweli kama ulivyosikia ila nisingependa kuzungumzia kila kitu kwa sasa nahitaji kupumzisha akili,” alisema Mbasha.
Mbasha aliyetoka kwa dhamana Juni 19, katika kesi hiyo ya kudaiwa
kubaka iliyosomwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, kesi yake itatajwa
tena Julai 17, mwaka huu.
No comments:
Post a Comment