HABARI zilizotua kwenye meza ya Uwazi juzi zinadai kuwa familia mbili, ya Emmanuel
na Flora Mbasha zimeweka kikao kwa siku tatu mfululizo kutaka kuinusuru
ndoa ya wawili hao lakini imeshindikana huku pembeni ikidaiwa kwamba
ili mambo yakae sawa lazima Mbasha alipe shilingi milioni 60.
Mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili Bongo Flora Mbasha.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, kikao hicho kiliitishwa na baba wa Mbasha kwa kushirikiana na ndugu wengine wa pande zote mbili.
“Mbasha na mke wake, Flora walikutanishwa sehemu fulani jijini Dar es
Salaam kwa ajili ya kupatanishwa. Kikao kilikuwa kizito, wakubwa wa
familia zote walikuwepo lakini Flora alikataa mara tano kurudi kwenye ndoa yake.
UWAZI LAPIGA HODI NYUMBANI KWA MBASHA
Juzi Jumapili, Uwazi
lilitia timu nyumbani kwa Mbasha, Tabata-Kimanga jijini Dar na
kubahatika kuzungumza na baba na mama wa Mbasha bila kumpata Mbasha
mwenyewe.
Mzee huyo aliyejitambulisha kwa jina la Maneno alikiri kuwepo kwa
kikao kwa muda wa siku tatu tofauti lakini akasema mambo yalishindikana.
“Mimi nilikuja Dar kutokea Dodoma wiki moja iliyopita baada ya kupata
wito wa mwanangu kuhusu mgogoro wa ndoa. Nilipofika hapa, sikumkuta
Flora, nyumba ilikuwa tupu.
“Kikao kiliitishwa na pande zote mbili, akiwemo Mchungaji Gwajima
ambaye alionekana kusuluhisha mgogoro wao lakini dalili za Flora
hazikuonesha kuwa tayari kurudi kwenye ndoa yake,” alisema mzee huyo.
Emmanuel Mbasha.
KUNA MKONO WA MTU
Mzee Maneno aliendelea kusema: “Mimi kama mtu
mzima, nilichokiona katika ndoa ya mwanangu kuna mkono wa mtu. Ila sasa
ametumia mbinu kubwa sana kumrubuni Flora na yeye kakubali kurubunika.”
MAMA MZAZI NAYE
Kwa upande wake, mama mzazi wa Mbasha, Zulfa
Maneno alisema kwake ni masikitiko makubwa kwa sababu mtoto wake
alishakuwa na jina kubwa kimataifa na mkewe pia.
Alisema: “Mimi kwenye kikao nilipomwona Flora anakataa ndoa yake mara tano, kila akiulizwa anasema hataki kurudi mpaka mara tano, nikajua hakuna ndoa.
“Ninachojua, mgogoro huo wa ndoa ulitengenezwa kwa makusudi kabisa
ili ndoa ivunjike. Ila kama aliamua kumwacha mwanangu angefanya hivyo
kwa amani na si visa kama hivi.”
Kuhusu kutakiwa shilingi milioni sitini ili Flora arejee kwenye ndoa
yake, wazazi hao walisema hawajui kitu labda kama yanasemwa pembeni.
Baba mzazi wa Emmanuel Mbasha.
KULIKUWA NA MGOGORO Habari zaidi zinadai kwamba, fedha zinazotakiwa
kulipwa ni kwa sababu, ndoa hiyo ilikumbwa na mgogoro kabla ya kuibuka
kwa madai ya Mbasha kumbaka shemeji yake.
Flora aliwahi kufungukia
hilo kwamba, kabla ya kutokea kwa madai ya ubakaji, alitibuana na Mbasha
na akaamua kuondoka nyumbani kwenda kuishi hotelini.
DALILI MBAYA
Kuna madai kwamba, siku ambayo Mbasha alikwenda
kujisalimisha polisi (Juni 16, 2014), Flora alipigiwa simu kujulishwa
lakini hakutokea kituoni.
Ikazidi kuelezwa kwamba, siku Mbasha anapelekwa Mahakama ya Wilaya ya
Ilala, Dar kujibu madai ya ubakaji, pia Flora alijulishwa lakini
hakutokea mahakamani hapo.
Mbali na kupelekwa mahakamani, habari za uhakika zinasema hata pale
Mbasha alipokosa dhamana na kupelekwa kwenye Gereza la Keko, Flora
alijulishwa, lakini hakufanya lolote.
“Je, kwa hayo yote ni kweli Flora anaipenda ndoa yake? Si jibu lipo wazi kwamba hakuna ndoa.” alisema mtu mmoja aliye karibu na familia hiyo.
Mama mzazi wa Emmanuel Mbasha.
MBASHA BAADA YA KUTOKA JELA
Ushahidi wa majirani umeweka bayana
kwamba, Mbasha alipotoka gerezani na kufika nyumbani kwake,
Tabata-Kimanga, Dar, walimfuata na kuangua kilio mbele yake huku wakimpa
pole kwa mkasa mzima.
Baadhi ya majirani waliozungumza na Uwazi juzi, walisema kuwa siku
hiyo nyumbani kwa Mbasha kulikuwa na dalili zote za kuwepo kwa msiba
kwani vilio vilitawala.
MADAI
Mbasha, alipandishwa mahakamani Juni 17, mwaka huu kwa madai ya kumbaka mara mbili shemeji yake (jina tunalo).
Siku hiyo alikosa dhamana na kupelekwa Gereza la Keko ambapo Alhamisi
ya Juni 19, mwaka huu alirudishwa tena mahakamani hapo kwa ajili ya
dhamana. Kesi yake itaanza kusikilizwa Julai 17, mwaka huu huku
ikielezwa kuwa upelelezi umekamilika.
No comments:
Post a Comment