Hii inatokea wakati bado kuna wasiwasi mkubwa juu ya hatma ya
wasichana zaidi ya 200 waliotekwa nyara na kundi hilo yapata siku 50
zilizopita.
Wakaazi wa kijiji cha Attagara
karibu zaidi na mpaka wa Cameroon na Nigeria wamesema kuwa watu
waliovalia sare za kijeshi walikuja katika kijiji chao na kuwaagiza watu
waje katika uwanja wa kanisa.
Wanadai kuwa walidhania watu hao walikuwa
wnajeshi wa serikali waliokuja kuwapa ulinzi. Na baada ya wanajeshi hao
kuwafyatulia risasai ndipo waligundua kuwa walikuwa wapiganaji wa Boko
Haram.
Mbunge wa eneo hilo Peter Biye amethibitishia
BBC tukio hilo na kusema kuwa watu wengi wameuawa na nyumba kuchomwa
katika vijiji vingine 5 mbali na hicho.
'Jeshi lakanusha madai'
Wakati huo huo jeshi la Nigeria limekanusha
madai katika vyombo vya habari kuwa mahakama ya kijeshi nchini humo
imewapata na hatia baadhi ya maafisa wakuu wa jeshi kwa kuwasaidia
wapiganaji wa Boko Haram.
Msemaji kutoka jeshi hilo amekanusha madai kuwa kuna majenerali 15 wa wa jeshi waliofunguliwa mashtaka ya kuwasaidia magaidi.
Jeshi limesema kuwa taarifa hizo ni batili zilizolenga kulidhalilisha jeshi la nchi hiyo wakati mambo yako tete.
nyumba zimechomwa Borno
Hali imeendelea kuwa ya wasiwasi miongoni mwa wakaazi wa maeneo mengi
kaskazini mashariki mwa Nigeria kutokana na mashambulio yaliyochacha.
Wapiganaji wamekuwa wakishambulia kwa bomu maeneo ya umma na kuwaua watu zaidi ya 200 katika chini ya miezi miwili tu.
Suala la wasichana waliotekwa pia bado limekaa
kama mwiba wa samaki kooni mwa serikali ya Nigeria ambapo shinikizo
kutoka jamii ya kimataifa zinaendelea kutaka wakombolewe kwa haraka.
Awali serikali ilikuwa imepiga marufuku
maandamano yoyote kutokana na tisho la usalama lakini ssa polisi
wametangaza kuwa maandamano ya amani yanaweza kufanywa.
KWA HISANI YA BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment