‘UCHAWI’ umetajwa kwenye mapenzi ya staa wa filamu Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ na ubavu wake wa sasa, Chuchu Hans.
Staa wa filamu Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ akiwa na mpenzi wake Chuchu Hans.
Kwa mujibu wa vyanzo vyetu, mapenzi ya Ray kwa Chuchu ni makubwa sana
kiasi kwamba hayawezi kuwa ya hivihivi tu kwani msichana huyo ni mtoto
wa Kitanga anayejua jinsi ya kumshika mwanaume kama Ray.
“Unajua siku moja niliongea na mtu, sitaki kumtaja jina. Akasema
anaamini mambo ya ‘kiswahili’ yapo katika mapenzi ya wawili hao, si
rahisi Ray akawamwaga akina Johari (na Mainda) na kubaki na Chuchu tu.
“Yule Chuchu ni mtoto wa Kitanga, watoto wa Kitanga ni waja leo
waondoka leo, wanajua mambo mengi sana kuhusu mapenzi, wapo akina
Mwakipesile walikwenda Tanga kufuata biashara ya nazi hawakurudi Mbeya,”
kilisema chanzo hicho.
“Kama mtakumbuka waandishi, siku moja kwenye magazeti yenu mliandika
kwamba Ray amesema hana mpango wa kumuoa Chuchu, lakini juzi tu kamvisha
pete ya uchumba kwa hiyo sasa uchumba wao ni rasmi.
“Halafu kama mtakumbuka tena katika habari ileile, mlimuuliza Chuchu
kuhusu madai ya Ray kwamba hana mpango wa kumuoa, alijibu Ray hana ubavu
huo, yaani wa kutomuoa. Sasa niambieni, mtu ambaye hana mpango wa
kumuoa demu, kwa nini amvishe pete ya uchumba?” kilihoji chanzo.
Kikaendelea: “Hata kwenye tasnia ya filamu, wengi wanasema mapenzi ya
Ray na Chuchu yana ‘kamzizi’ si bure maana jamaa ameoza kuliko
inavyotakiwa.”
Baada ya taarifa hizo, juzi Amani lilimsaka Ray na kubahatika
kukutana naye kwenye Gym moja iliyopo Kinondoni jijini Dar ambapo
alipoulizwa kuhusu madai hayo hakupenda kutoa ushirikiano wowote ule,
akasingizia anawahi hospitali ana Homa ya Dengu.
Chuchu alipatakana nje ya Meeda Club Jumamosi iliyopita ambapo alipoulizwa alisema:
“Kwanza nyiye mbona mnapenda sana kuwafungukia watu bila wao kujifungukia wenyewe? Acheni watu wafunguke wenyewe bwana.”
Hata hivyo, ni kweli Chuchu Hans ana pete ya uchumba kwenye kidole kinachohusika.
Credits to Global Publishers
No comments:
Post a Comment