Thursday, May 15, 2014

TAZAMA HAPA JINSI UKAWA WALIVYOTEMBEZA KICHAPO MOROGORO










Mwenyekiti wa Bavicha, John Heche akithibitisha kumtambua kijana huyo anayedaiwa kushiriki kumteka mbunge wao kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika Jimbo la Kalenga, lringa.

Mmoja wa viongozi wa Chadema mkoa wa Morogoro, lnnocent Zawadi ambaye alikuwepo jimboni Kalenga naye akithibitihsa pia kumtambua kijana huyo.


NJEMBA mmoja amepokea kipigo kikali kutoka kwa wafuasi wa Ukawa waliokuwa na mkutano mkoani Morogoro jana Jumatano jioni baada ya kudaiwa kuwa miongoni mwa waliomteka Mbunge wao, Rose Kamli wakati wa uchaguzi mdogo jimboni Kalenga, mkoani Iringa.
Njemba huyo ambaye hakufahamika jina lake mara moja, aliangushiwa kipigo kikali baada ya kuibuka na kuanza kumpiga picha Mwenyekiti wa Bavicha Taifa, John Heche. Baada ya kipigo cha nguvu, njemba huyo alinusuriwa na polisi waliomchukua kumtoa mikononi mwa wafuasi hao.
Mwenyekiti huyo wa Bavicha akithibitisha kumtambua kijana huyo anayedaiwa kushiriki katika kumteka mbunge wao na kumpiga kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika Jimbo la Kalenga, lringa mwezi uliopita.

No comments:

Post a Comment