Wednesday, May 14, 2014

LIVEEEE: TAZAMA HAPA MWANAMKE KIBAKA ALIVYOBAMBWA BAADA YA KUKWAPUA BUKU 20.

Umati wa watu ukiwa unashangaa kitendo cha mwanadada (kushoto mwenye kitambaa cha zambarau kichwani) aliyemkwapulia 20,000 mwenzake. 

Wengine wakitaka apigwe kama mwizi, wengine wakiomba asamehewe.

 Mwanadada aliyeiba 20,000/= huyu hapa.

 Vijana wakimkingia kifua asipigwe.


 Vijana wakiondoka naye kwenda kusikojulikana.


MWANADADA mmoja ambaye jina lake halikufahamika amejikuta akinusurika kupigwa na wananchi wenye hasira kali baada ya kumuibia mama aliyekuwa na mtoto.
Ishu nzima imetokea maeneo ya jirani na hospitali ya Amana, Ilala, jijini Dar es Salaam, ambapo  baada ya mama mmoja aliyekuwa na mtoto kumkabidhi mwanadada (mwizi) mtoto na mkoba wake, ndipo mdada huyo alipochomoa shilingi 20,000/= kwenye mkoba wa mama huyo.
Aliporudi mama wa mtoto alimkabidhi mtoto na mkoba wake kisha kuondoka kwa haraka na wasiwasi mwingi, kitu kilichomshitua yule mama na kujisachi ndipo alipobaini kuibiwa na kuanza kupiga kelele za mwizi.
Vijana walionyesha uwezo wao kwa kumkimbiza na kumkamata ambapo alinyang’anywa pesa na zogo likaibuka wakati wengine wakitaka kumpiga huku baadhi ya vijana wakionekana kumkingia kifua kwa kuwa ni mwanamke.

Credits to Global Publishers.

No comments:

Post a Comment