Kijana aliyefahamika kwa jina la Samson Ntemi aliyetuhumiwa kwa utapeli wa madini bandia
Kwa mujibu wa chanzo makini, mtu huyo alianza harakati za utapeli wake kwa kumpigia simu mfanyabiashara mmoja wa magari akimweleza kuhusu nia yake ya kununua gari aina ya Canter kutoka kwake kwa kiasi cha shilingi milioni 32.
Chanzo kilisema kufuatia simu mfululizo za mtu huyo, mfanyabiashara huyo alipata hofu na kuhisi huenda alikuwa ni tapeli, hivyo kuweka mtego na kumtaka wakutane Mwananyamala kwa ajili ya kufanya biashara hiyo.
Madini bandia aliyokutwa nayo Samson Ntemi
Lakini hata hivyo, walipokutana tapeli huyo alimtaka mfanyabiashara huyo kuongozana naye hadi Kurasini, akidai ndipo alipokuwa mteja mwenye kulihitaji gari hilo.
“Nilishangaa jamaa akinibadilishia kauli akidai anayetaka gari ni bosi wake siyo yeye.
Nilipomhoji vizuri akaniambia yeye ni mfanyabiashara wa madini kutoka Mahenge, Ifakara, mkoani Morogoro aliyefika Dar kutafuta soko huku akionesha kutolijua vizuri Jiji la Dar,” chanzo chetu kilimnukuu mfanyabiashara huyo akisema.
Inadaiwa kuwa tapeli huyo alimwonyesha mfanyabiashara huyo madini hayo yenye thamani ya mamilioni ya shilingi na kumtaka anunue. Baada ya kuyaona na kugundua kuwa ni feki, alimtaka tapeli huyo kuandamana naye hadi benki maeneo ya Kijitonyama ili amkabidhi.
Wakiwa njiani, mfanyabiashara huyo aliwasiliana na Polisi wa Kituo Kidogo cha Mabatini, Kijitonyama ambao walikuja eneo la tukio na kumkamata tapeli huyo, aliyekiri mbele ya askari kuwa alishawahi kufanya wizi huo katika miji ya Tarime, Arusha na Shinyanga.
Global Publishers
No comments:
Post a Comment