Mbovumbovu za staa! Miss Ruvuma 2006, Isabela Mpanda amedhihirisha jinsi
alivyo hamnazo baada ya kuvua nguo hadharani na kuacha nyeti nje bila
kujali watu waliokuwa wakimshangaa.
Isabela Mpanda akimwaga radhi ukumbini.
Tukio hilo la kushangaza lilitokea Alhamisi iliyopita kwenye Ukumbi
wa Mawela uliopo Sinza, Dar ambako kulikuwa na kitchen party ya
mwigizaji, Vanita Omary ambapo Isabela aliwashangaza watu baada ya
kuacha nyeti nje.
Bila chembe ya aibu, Isabela akivalia gauni fupi akiwa tilalila,
alikuwa akicheza muziki huku akilinyanyua gauni juu na kuacha sehemu
nyeti za makalio nje na kusababisha ‘kufuli’ yenye muundo wa bikini
kuonekana.
Miss Ruvuma 2006, Isabela Mpanda wakati akiingia ukumbini.
Ishu hiyo ilizua minong’ono kwa baadhi ya wageni waalikwa na kubaki wakimshangaa kwa kitendo hicho na kudai kuwa ni hamnazo.
Akiwa anafanya tukio hilo la kujifunua alisikika akisema amepania
sherehe hiyo kwani yeye ndiye wifi wa Vanita na kama mwigizaji
Jacqueline Wolper aliacha kufuli lake kubwa wazi na yeye aliamua
kuonyesha lake aina ya bikini nje ili lionekane kwani ni la bei kubwa.
Isabela Mpanda akinyonyana ndimi na baby wake Luteni Kalama.
“Mh, kweli huyu Isabela hamnazo yaani anajifunua mbele za watu, hata
haogopi, ukweli anatia aibu lakini afadhali wanaume hawapo maana
wangekuwepo ingekuwa aibu zaidi,” walisikika wasanii wawili
wakijadiliana huku wakimkodolea macho mwanadada huyo.
No comments:
Post a Comment