Thursday, August 14, 2014

AJALI MBAYA ARUSHA, NI GARI NDOGO ILIYOTUMBUKIA MTONI.... DEREVA AFARIKI HAPO HAPO

Gari aina ya Toyota Verosa iliyotumbukia mtoni majira ya saa nane usiku wa kuamkia leo karibu na Premier Casino Arusha! Mtu mmoja aliyekua akiendesha alifariki hapohapo. Mpaka sasa bado haijajulikana jina la dereva wa gari hilo ambaye amepoteza maisha katika ajali hiyo mbaya.

Gari aina ya Toyota Verossa yenye namba za usajili T129BTY ikiwa mtoni baada ya kupinduka na kutumbukia.



Baadhi ya mashuhuda wakiangangalia gari hiyo ikiwa mtoni .

No comments:

Post a Comment