Wednesday, July 2, 2014

TAZAMA PICHA ZA TUKIO LA KUSHAMBULIWA BASI LA MAGEREZA NA MAJAMBAZI

BASI la Jeshi la Magereza lililokuwa na mahabusu likitokea Mahakama ya Kawe jijini Dar es Salaam, limeshambuliwa na watu wenye silaha waliokuwa kwenye pikipiki.
Inadaiwa kuwa watu hao walitaka kumdhuru mtu aliyekuwa kwenye gari lililokuwa mbele ya basi hilo.
Walipoliona basi hilo wakadhani kuwa lazima kutakuwa na askari wenye silaha ndipo wakalishambulia.
Katika shambulio hilo, dereva wa basi na askari mmoja wamejeruhiwa na hakuna mahabusu aliyetoroka wala kujeruhiwa.



 Kioo cha nyuma cha basi hilo kilivunjika chote baada ya kushambuliwa kwa risasi.






Maeneo ya vioo vilivyoshambuliwa kwa risasi katika tukio hilo

Tundu la risasi katika kioo cha dirisha la mbele

No comments:

Post a Comment