Mwenyekiti wa kikundi cha
wanawake wafanyakazi wa Airtel Tanzania ‘Airtel Diva’, Amitin Mbamba
(kulia), akikabidhi msaada wa machela za kisasa mbili, ‘wheel chair’
mbili na bidhaa mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya milioni 5/-, kwa
Muuguzi Mkuu wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI), Mary Haule,
kwa ajili ya matumizi ya wagongwa katika taasisi hiyo, jijini Dar es
Salaam mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia ni wanachama wa Airtel Diva.
Mwenyekiti wa kikundi cha
wanawake wafanyakazi wa Airtel Tanzania ‘Airtel Diva’, Amitin Mbamba
(kulia), akikabidhi msaada wa moja kati ya ‘wheel chair’ mbili, machela
za kisasa mbili na bidhaa mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya milioni
5/-, kwa Muuguzi Mkuu wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI), Mary
Haule, kwa ajili ya matumizi ya wagongwa katika taasisi hiyo, jijini Dar
es Salaam mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia ni wanachama wa Airtel Diva.
Mkuu wa Taasisi ya Saratani ya
Ocean Road (ORCI), Mary Haule (kulia) akiwaongoza wanachama wa kikundi
cha wafanyakazi wanawake wa Airtel Tanzania ‘Airtel Diva’, wakati
walipotembelea wagonjwa wa taasisi hiyo, baada ya kukabidhi msaada wa
machela za kisasa mbili, ‘wheel chair’ mbili na bidhaa mbalimbali vyenye
thamani ya zaidi ya milioni 5/-, kwa ajili ya matumizi ya wagongwa
katika taasisi hiyo, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Wanachama wa kikundi cha
wafanyakazi wanawake wa Airtel Tanzania ‘Airtel Diva’, wakiwa wamebeba
bidhaa mbalimbali, walipotembelea wagonjwa katika Taasisi ya Saratani ya
Ocean Road (ORCI) na kukabidhi msaada wa machela za kisasa mbili, wheel
chair mbili vyenye thamani ya zaidi ya milioni 5/-, kwa ajili ya
matumizi ya wagongwa katika taasisi hiyo, jijini Dar es Salaam mwishoni
mwa wiki.
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kupitia umoja wa wanawake
ujulikanao kama Airtel Divas umetoa msaada wa vifaa vya hospitali
kwaajili ya wagonjwa wanaosumbuliwa na magonjwa ya saratani katika
hospitali ya Ocean road jijini Dar es salaam
Msaada huu unafatia harambee kwa ajili ya kuchangisha pesa
iliyofanywa na Airtel Diva mwezi uliopita kwaajili ya kupata fedha za
kuwasaidia wagojwa wanaosumbuliwa na magonjwa ya kansa katika hospitali
ya Ocean Road.
Akiongea wakati wa kutoa msaada huo mwenyekiti wa Airtel Divas Amitin
Mbamba alisema” Tunatambua na tunapokea kwa machungu matatizo
yanatowapata wanawake na watoto wanaougua saratani na katika kuadhimisha
siku ya wanawake duniani kwa mwaka 2014 tuliamua kuchangisha pesa
kwaajili yakutuwezesha kununua vifaa vya hospitali na kuwasaidia
wanawake na watoto pamoja na wagonjwa wengine hospitalini hapa.
Na leo tunayofuraha kutoa stretcher 2 pamoja na wheelchair 2 zenye thamani ya shilingi million 5 hospitalini hapa.”
Tunaamini msaada huu utawawezesha wahudumu kupata nyenzo muhimu na
kuweza kufanya kazi yao ya kutoa huduma kwa wagojwa kwa ufanisi zaidi.
“Nia yetu ni kuhakikisha tunaendelea kutoa muda wetu na rasilimali
katika kushikiri na kuchangia shughuli za huduma kwa jaimii ili
kukubailiana na matatizo yanayoikumba jamii inayotuzunguka hususani
wanawake wenzetu” aliongeza Mbamba
Mmoja ya wajumbe wa Airtel Divas Bi Deliphina Martin Msuya alisema”
tunayofuraha kuwa sehemu ya kutoa msaada kwani tunatambua umuhimu wa
wanawake katika kusimamia familia, inagusa sana kuona jinsi gani
wanawake wenzetu wanavyougua au kuuguza watoto wao hospitalini hapa
hivyo tunatoa wito kwa wanawake wengine huku nje mmoja mmoja au kwa
makundi kuwasaidia wanawake wenzetu walio katika changamoto hizi kwani
ni jukumu letu kusaidia wahitaji.
Akiongea mara ya kupokea msaada huo Muuguzi Mkuu wa Taasisi ya
Saratani ya Ocean Road (ORCI), Mary Haule alisema” Hospitali yetu
inaupungufu wa vifaa mbalimbali zinavyotuwezesha kuhudumia wagonjwa
tunashukuru sana Airtel kwa msaada wao na kwa kuwezesha kupata hivi
vifaa kwani vitatusaidia katika kutoa huduma na kuongeza ufanisi wa kazi
zetu za kusaidia wagonjwa hapa hospitalini.
Nachukua nafasi hii kuwaomba makampuni mengine na vikundi mbalimbali kusaidia changamoto zingine zilizopo hospitalini hapa.
Airtel Divas ni mpango ulioanzishwa Airtel Afrika nzima wenye lengo
la kuwahamashisha na kuwawezesha wanawake wanaotoka katika makuzi , mila
na tamaduni mbalimbali kujiamini na kufanikiwa katika maisha , mpango
huu ulizindulia Airtel Tanzania March 2012.
No comments:
Post a Comment