Makamu wa Rais wa Pili wa
Zanzibar, Balozi Sefu Ali Iddi akisalimiana na baadhi ya wageni
alipowasili kwenye ufunguzi wa Tamasha la 17 la ZIFF Kulia ni Mwenyekiti
wa Bodi ya ZIFF Mh. Mahmoud Thabit Kombo.
Mgeni rasmi Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar, Balozi Sefu Ali Iddi akisalimiana na Mgeni maalum
mwalikwa mwigizaji wa filamu ya MANDELA "Long Walk to Freedom" Terry
Pheto ambayo ilifungua tamasha hilo la 17 la ZIFF usiku wa kuamkia leo
visiwani Zanzibar.
Mwenyekiti wa Bodi ya ZIFF, Mh. Mahmoud Thabit Kombo akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Wananchi Group ambao ni wadhamini wa ZIFF kupitia ZUKU, Bw. Mohammed Jeneby wakati wa tamasha hilo.
Pichani juu na chini ni kikundi cha burudani cha TANURI kutoka Egypt wakitoa burudani kwenye tamasha la 17 la ZIFF.
No comments:
Post a Comment